Search This Blog

Friday, February 8, 2013

SAMATTA: GOLI LANGU DHIDI YA CAMEROON NI OMBI LANGU LA MSAMAHA KWA WASHABIKI NA NAAMINI WAMENISAMEHE

MBWANA Samatta amesema kuwa anaamini goli la ushindi alilofunga dhidi ya Cameroon linatosha kumsafisha kwa mashabiki wake.
 

Hiyo imekuja baada ya mashabiki wa soka kuwazomea pamoja na Thomas Ulimwengu wakati Stars ikicheza na Zambia, mwaka jana kwenye uwanja wa Taifa.
 

Nikutokana na kuchelewa kuripoti kambini kujiwinda na mchezo huo wa kirafiki na Chipolopolo mwakajana.
 

Kitendo hicho kilimkasirisha kocha Kim Poulsen ambaye aligoma kuwapanga kwenye kikosi ambacho kilicheza mtanange huo.
 

Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0. Bao hilo pekee, likizamishwa na Mrisho Ngassa kwa shuti la mwendo mrefu.
 

"Naamini ushindi huu utakuwa umewafurahisha mashabiki na kurudisha imani kwetu." alisema Samatta.
 

Alisema haikuwa lengo leo kuchelewa kujiunga na kambi ya timu isipokuwa ni mambo tu yaliingiliana.

6 comments:

  1. safi jembe endelea kukaza

    ReplyDelete
  2. In normal situation everyone do mistake but what is important is to go back and see what make u to do such a mistake in addition to that is to go further or a greater distance and say sorry! we appreciate u, Mbwana Sammata"Golden boy" we will never judge u! this make me remember the beautiful quote from mother teresa"If you judge people,u have no time to love them"

    ReplyDelete
  3. kaza buti, ila kama kweli ilikuwa pozi achana nazo zitakuharinia

    ReplyDelete
  4. Shafih,Mimi ninaomba ujumbe wangu uwafikishie Watanzania kuwa Timu ya Taifa ikiwa inacheza wapenzi tuvae jezi ya Timu ya Taifa,huwa sipendi kuona Timu ya Taifa inacheza alafu wapenzi wanavaa jezi za timu zao za Simba na Yanga,napenda kuwakumbusha kuwa Jezi za Klabu zinasehemu yake na Jezi ya Taifa inasehemu yake.

    ReplyDelete
  5. Dah! Bongo noma, yaan sasahv imekuwa safi hiyo kisa goli! Je acngefunga? Achen ulimbuken bhana. Ww dogo hayo yalipita na hatutegemei upuuzi wa hivyo tena ujirudie swala la msingi n kuwa commited, unadhan Amenike na Odemwingie wanalingana? Nan anaheshimika kwa sasa? Jupangen!

    ReplyDelete