Search This Blog

Friday, February 8, 2013

RIGOBERT SONG: DHARAU NA KUJIAMINI KUPITA KIASI KUMEFANYA STARS WATUFUNGE


RIGOBERT Songs amesema dharau na kujiamini kupita kiasi ni vitu ambavyo vilichangia Taifa Stars kuifunga Cameroon katika mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Taifa jana.
 

Stars ilishinda bao 1-0. Bao hilo likifungwa na Mbwana Samatta aliyeunganisha krosi ya Frank Domayo dakika 89 ya mchezo.
 

Meneja huyo alisema jijini Dar es Salaam kuwa Taifa Stars ilicheza vizuri lakini wachezaji wake walikosa umakini.
 

"Ukiangalia goli ambalo tulifungwa utafahamu hilo. Mabeki hawakuwa makini."
 

Alisema wakati Domayo anapiga krosi beki wa kushoto Assou Ekotto alikuwa akimtazama na mpira huo kutua kwenye miguu ya Samatta aliyetikisa nyavu za Cameroon kirahisi.
 

"Hatukuwa makini. Mazingira ya goli yenyewe yanajieleza." alisisitiza beki huyo wa zamani wa Cameroon na Liverpool ya England.

5 comments:

  1. Huenda ni kweli lakini nadhani Stars walijuwa watanzania tunataka nini? Hongereni Stars!
    NURU SPORTS MSM

    ReplyDelete
  2. Stars wako juu huo ukweli lazima tuukubali.....wanatandaza bolo ka Barcelona!..hureee Stars.....hamna cha kujiamini sana au dharau..Cameroon walizidiwa lazima wakubali....!

    ReplyDelete
  3. This is just the commencement towards myriads of success, we are capable enough to humiliate them in their home ground with their huge turnout!!!!! they did not look down on Taifa stars but rather Taifa stars is now among of the most formidable team with youth having thirst of achievements. So song is absolutely not right. hallaaa Taifa stars, best discipline will take u to the next step.

    ReplyDelete
  4. cameroun choka mbaya sasa hv,tunalingana tu kwa kiwango,iweje watudharau bana,hawakujua kuwa tuko level moja?ndo maana wote hatujaenda south

    ReplyDelete
  5. kuna faida gani kuwafunga zambia comeroun, brazil hata italy katika mechi za kirafiki halafu tunakosa afcon kila siku ... thats jokes bado kabisa safari ndefu tumeachwa hapahapa na burkina faso, carpe varde

    ReplyDelete