Search This Blog

Saturday, November 26, 2011

EXCLUSIVE: KOCHA MPYA WA SIMBA KUWASILI LEO BONGO


Baada ya aliyekuwa kocha wa timu ya Simba Moses Basena kutemeshwa kibarua chake kwa kukosa kibali cha kufanya kazi nchini, klabu hiyo inatarajiwa kupata kocha leo. Boss mpya wa benchi la ufundi la Simba, Mserbia Milovan Cirkovic, anatarajiwa kuwasili nchini leo, kabla ya kesho kusaini mkataba wa kuinoa timu hiyo kwenye Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.

Hii ni mara ya pili kwa Milovan kuja kuinoa timu hiyo ambapo awali aliifundisha mwaka juzi kabla ya kuiacha na nafasi yake kushikwa na Mzambia, Patrick Phiri.

Makamu Mwenyekiti wa Simba, Goefrey Nyange ‘Kaburu’, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa, Milovan ambaye anambadili Mganda Moses Basena, anawasili leo usiku na pindi atakaposaini mkataba huo, atabaki kuendelea na shughuli nyingine.

Alisema walishafanya mazungumzo na kocha huyo na hivyo ujio wake unatokana na makubaliano waliyoafikiana baina yao.

1 comment:

  1. Jamaa alikuwa Kocha mzuriila alifanya kayi nawababaishaji, kama kweli atatua nchini basi anaweza leta mabadiliko kwenye klabu ya simba ila wamlipe mshahara waache utani. Jambo Simba wangempa hiyo time King Kibadeni Mputa ni kocha mzuri pia na mwenye uzoefu na soka la bongo.
    Mike

    ReplyDelete