Search This Blog

Saturday, November 26, 2011

MIZENGO PINDA KUTINGA TAIFA LEO KUWAPA SAPOTI KILI STARS.

Kiranja Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa michuano ya CECAFA Chalenji 2011 ambapo wenyeji Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ wataumana na Rwanda ‘Amavubi’ kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema, Pinda angezindua michuano hiyo iliyoanza jana kwenye uwanja huo.

Kilimanjaro Stars inayonolewa na Charles Boniface Mkwasa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ambao ndio mabingwa watetezi, itashuka katika dimba hilo kukuvaana na Rwanda majira ya saa 10:00 jioni.

Michuano hiyo ilianza jana ambapo Burundi iliitandika Somalia mabao 4-1, katika mchezo wa kwanza, huku Uganda ikifunga Zanzibar mabao 2-1 katika mchezo wa pili.

Katika hatua nyingine, TFF imetangaza viingilio katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ambapo kwa mashabiki watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo ni zaidi ya 30,000 kiingilio kitakuwa sh 1,000, wakati viti vya rangi ya chungwa zaidi ya 10,000 kiingilio kitakuwa sh 3,000.

Wambura alisema kwa watakaokaa VIP C na B ambayo jumla ya viti vyake ni 8,000 kiingilio kitakuwa sh 5,000 wakati VIP A yenye viti 700 kiingilio ni sh 10,000.

1 comment:

  1. TFF waache kutangaza viingilio kwa kutenganisaha majukwaa. Ukiingia uwanja wa Taifa utakuta watazamaji waliokaa VIP ni wale waliolipa shilingi elfu mbili au elfu moja badala ya wale waliolipa shilingi elfu ishirini!!! Kuna haja gani sasa ya TFF kutenganisha majukwaa na gharama za kiingilio wakati watu wanaokaa sio wale wanaotakiwa kukaa hapo!

    ReplyDelete