Search This Blog

Saturday, November 26, 2011

CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP: ZANZIBAR YAANZA KWA KIPIGO

Mchezaji wa Zanzibar Heroers Ali Badru akichuana na mchezaji wa Uganda Cranes Andrew Mwesigwa wakati timu hizo zikichuana katika mchezo wa kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP

Waziri Mkuu wa Kenya Bw. Raila Odinga katikati akifurahia jambo kwa pamoja na Rais wa Shirikisho la vyama vya Michezo Afrika Mashariki Leodger Tenga kushoto pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mutinda Mutiso wakati walipkuwa wakishuhudia pambano la pili katika mashindano ya kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 linalofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Tayari mpira umekwisha ambapo Uganda Cranes imeifunga Zanzibar Heroers magoli 2-1 goli la kwanza la Uganda Cranes limefungwa na Mchezaji Danny Wagaruka katika kipindi cha kwanza, huku Mike Serumaga akifunga goli la pili katika kipindi cha pili, goli la kufutia machozi kwa upande wa Zanzibar Heroers limefungwa na mchezaji Ali Badru katika kipindi cha pili.

Wadau kutoka Serengeti Breweries nao walikuwepo kwani wao ndiyo wawezeshaji au wadhamini wa mashindano haya mtari wa juu kutoka kulia ni Moses Keba, Mr. Ssebo, mstari wa chini kutoka kulia ni Ritah Mchaki na Maurice Njowoka

Kocha Micho ambaye amewahi kuifundisha Yanga sasa ni kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda- nae alikuwepo uwanjani kuangalia mchezo

Wadau na mashabiki wa soka wakiwa wanatizama mchezo huo wa ufunguzi wa CECAFA Tusker Cup.

No comments:

Post a Comment