Search This Blog

Friday, November 25, 2011

BECKHAM MBIONI KUJIUNGA NA PSG KWA £12M


David Beckham yupo katika mazungumzo ya mwisho ya kusaini mkataba wa kujiunga na Paris Saint-Germain baada ya kupewa ofa ya mkataba wa miezi 18 wenye thamani ya £12m.

Beckham amekuwa kipenzi cha raisi wa PSG Nasser al-Khelaifi anayemuona Becks kama mtu sahihi wa kuipa mageuzi klabu hiyo kuwa moja ya timu kubwa barani ulaya.

Jana Al-Khelaifi alikiri kwamba uamuzi wa timu gani ya kujiunga nayo ulikuwa kati ya Tottenham na PSG, lakini inaeleweka kuwa muingereza huyo anapendelea zaidi kujiunga na wafaransa hao.

Fedha sio tatizo kwa PSG na wana imani kubwa watafanikiwa kumshawishi Beckham kusaini mkataba wa kuitumikia klabu yao in January. Spurs hawawezi kupambana na matajiri wa kiarabu wanaoimiliki klabu hiyo, ukiachana na mshahara pia hana uhakika kama atapata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha Harry Redknapp.

PSG wametoa ofa hiyo nzuri katika mazungumzo yao yanayoendela kati yao na wawikilishi wa Becks na wanaamini watashinda mbio za kumsajili kiungo huyo.


No comments:

Post a Comment