Search This Blog

Friday, November 25, 2011

EXCLUSIVE: BASENA KUTOENDELEA KUIFUNDISHA SIMBA MSIMU HUU

*******************************KWAHERINI******************************************

Taarifa za kuaminika 100% ambazo blog hii imezipata ni kwamba kocha Moses Basena hatoendelea kuifundisha klabu ya Simba katika duru la pili la mzunguko wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Chanzo cha Basena kushindwa kuendelea na kazi katika klabu ya Simba ni kutokana na kukosa kibali cha kuendela kufanya kazi permanently nchini hali iliyopeleka klabu hiyo kushindwa kuendelea nae kama kocha mkuu wa ndani ya timu hiyo.

Simba kwa sasa wapo katika mchakato wa kutafuta kocha atakayeziba pengo la Basena na kuiwezesha klabu hiyo kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu na hatimaye kutwaa uchampion wa Tanzania bara.

1 comment:

  1. Juzi juzi nilisoma taarifa moja ikisema ametumiwa tiketi ya ndege na Kaburu akathibitisha kua ni kweli imekuaje tena so tetesi za replacement yake?.
    Mimi Rasheed Khalifa wa Sinza

    ReplyDelete