Search This Blog

Wednesday, November 23, 2011

HATMA YA TENGA CECAFA KUJULIKANA KESHO


Mkutano Mkuu wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) utafanyika kesho (Novemba 24 mwaka huu) kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam.
Moja ya ajenda katika mkutano huo utakaonza saa 4.00 asubuhi ni uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya CECAFA. Nafasi zinazogombewa ni tano; (Mwenyekiti na wajumbe wane wa Kamati ya Utendaji).
Wagombea uenyekiti ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ambaye anatetea nafasi hiyo. Mpinzani wa Tenga ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Djibouti, Fadoul Hussein.
Nafasi nne za Kamati ya Utendaji zinagombewa na watu wanane. Wagombea hao ni Abdiqani Saeed Arab (Somalia), Tariq Atta Salih (Sudan), Justus Mugisha (Uganda), Tesfaye Gebreyesus (Eritrea), Hafidh Ali Tahir (Zanzibar), Sahilu Wolde (Ethiopia), Raoul Gisanura (Rwanda) na Abubakar Nkejimana (Burundi).
Baada ya Mkutano Mkuu, saa 7.00 mchana kutakuwa na mkutano na waandishi wa habari ambao utafanyika hapo hapo hoteli ya JB Belmont.

No comments:

Post a Comment