Search This Blog

Friday, March 9, 2012

REKODI ZA LIONEL "MESSIAH" MESSI KATIKA NAMBA



 
Historia imeendelea kutengenezwa. Magoli matano ya Lionel Messi katika ushindi wa Barcelona wa 7-1 dhidi ya Bayern Leverkusen katika usiku wa jumatano ya jana ulimfanya Muargentina huyo kuandika historia mpya katika vitabu vya champions league.
Akiwa anakaribia kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye  zaidi katika msimu kwa Barcelona na kwa ligi ya mabingwa ulaya katika msimu mmoja – blog hii inakuletea rekodi za kijana huyu kutoka Argentina kupitia namba.

3 – Messi sasa amefunga hat tricks tatu katika ligi ya mabingwa wa ulaya, akiifika rekodi ya Filippo Inzaghi. Ni wachezaji watatu wa Barcelona (Rivaldo, Ronaldinho na Samuel Eto’o) ndio huko nyuma waliweza kufunga hat tricks katika kombe hilo. Pia amekuwa ndio mchezaji wa kwanza kufunga hat-tricks mbili katika msimu mmoja wa Champions league.


3 – Muargentina huyo alishinda tuzo mchezaji bora wa dunia mwaka huu, akiwafikia washindi wa zamani walioshinda mara 3 Michel Platin, Johan Cruyff na Marco Van Basten huku ndio kwanza akiwa na miaka 24.


4 – Messi amemaliza akiwa mfungaji bora wa Champions league katika miaka mitatu iliyopita. Na sasa yupo karibuni kuweza kumaliza msimu akiwa mfungaji bora na kuweza kufikia rekodi ya gwiji wa Bayern Munich Gerd Muller akiwa ndio mchezaji pekee  kuwa mfungaji bora kwa misimu minne mfululizo katika UCL/European Cup.


5 – Messi ndio mchezaji wa kwanza  katika historia ya Champions league kufunga magoli matano katika mechi moja.


6 – Mshambuliaji huyo mzaliwa Rosario amefunga katika mashindano sita tofauti kwa Barcelona msimu huu; La Liga, Copa del Rey, Spanish Supercopa, Uefa Super Cup na kombe la dunia la vilabu pamoja Champions league; akiifikia rekodi ya mchezaji mwenzie Pedro aliyoiweka 2009.


12 – Messi sasa amefikisha idadi ya magoli 12 katika champions league msimu huu, akiifikia rekodi yake aliyoweka msimu uliopita na akiwa yupo sawa na Ruud Van Nistelrooy aliyoiweka msimu wa 2002-03 – huku akiwa amebakiwa na michezo zaidi ya mitano kama Barca wafika finali msimu huu.


18 – Tangu aanze kuichezea Barcelona mwaka 2005, Messi ameshinda makombe  18 na wakatalunya hao.

22 – Kufuatia hat-trick dhidi ya Switzerland wiki iliyopita, Messi sasa ana magoli 22 katika mechi 67 alizoichezea Argentina. Diego Maradona alifunga magoli 34 katika mechi 91 akiwa na Albiceleste (Argentina).


24 – Katika mechi ya kwanza dhidi ya Leverkusen, Messi aliweka rekodi ya kufunga magoli mengi (19) katika hatua ya mtoano . Jana usiku akafunga mengine matano na kuifanya idadi hiyo kuongezeka hadi kuwa 24.


49 – Muargentina huyu sasa amefikisha jumla magoli ya champions legue 49 – akiwapita Del Piero (44), Filippo Inzaghi (46), Eusebio (47), Andry Shevchenko (48) katika listi ya wafungaji bora wa muda wote wa UCL na European Cup. Magoli yake matano  yalimfanya amkute gwiji wa Real Madrid Alfred Di Stefano wote wakiwa nafasi ya nne, nyuma ya Thierry Henry (51), Van Nistelrooy (54) na Raul (71).

93 – Messi ana assists 93 kwa Catalan club, zikiwemo 73 katika misimu minne iliyopita na 20 za msimu huu.

188 – Tangu Pep Guardiola achukue majukumu ya ukocha Barcelona, Messi amefunga mabao 188 katika mechi rasmi 201.

228 – Kwa ujumla, Muargentina huyo ana magoli 228 kwa klabu yake, akiwa nyuma kwamagoli 7 tu kuweza kufikia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote wa Barcelona Cesar Rodriguez.

1 comment:

  1. hakuna ka yeye tena coz in 24 yrs rekodi kibao

    ReplyDelete