Search This Blog

Saturday, June 15, 2013

MABADILIKO MAKUBWA KWENYE SHERIA ZA SOKA YAFANYIKA

Mkutano mkuu  wa 127 wa bodi ya vyama vya kimataifa vya soka (IFAB) ulifanyika huko Edinburgh (Scotland) tarehe 2 Machi 2013 . Mabadiliko ya sheria za mchezo wa soka yalipitishwa  kwenye mkutano huo pamoja na maelekezo kadhaa ambayo yameorodheshwa hapo chini.

Sheria za Mchezo na maamuzi ya bodi.

1.Sheria ya 11.- Tafsiri ya sheria za mchezo ( off side).

Mjadala wa ile dhana ya "kuingiliana na mpinzani wakati mchezo unaendelea yaani "Intefering with an opponent" pamoja na kujipatia faida kutokana na kitendo hicho yaani "ganing an advantage"

Dhana kwa jinsi ilivyo kwa sasa.

Katika mazingira ya sheria ya 11 ya kuotea au off side mambo yafuatayo huwa yanazingatiwa .

*"Interferring with play ina maana kuugusa mpira ambao umepigwa au kuguswa na mtu ambaye anatoka kwenye timu moja na mtu aliyeugusa .

* "interfering with an opponent" ina maana kumzuia mpinzani asicheze mpira kwa kukaa mbele yake makusudi kuzuia upeo wake wa kuuona mpira  yaani obstruction au kufanya vitendo au ishara ambazo kwa tafsiri ya mwamuzi vinaweza kumdanganya mpinzani au kumuondoa mawazo yake ya kuucheza mpira .

* "kujipatia faida kwa kuwepo kwenye nafasi husika kuna maana ya kucheza mpira ambao umedunda kwenye lango yaani rebound huku mfungaji akiwa kwenye eneo la kuotea .

Tafsiri mpya.

Katika mazingira ya sheria ya 11 , tafsiri zifuatazo zitazingatiwa .

* "kuingilia mchezo au interfiring with play" kunamaanisha Kuucheza au kuugusa mpira ambao umetoka kama pasi au umepigwa na mchezaji unaetoka naye timu moja "

* interferring with an opponent yaani kumzuia mpinzani asiucheze mpira inamaanisha kumzuia mpinzani asiwe kwenye uwezo wa kuucheza mpira kwa kumzuia kimwili pamoja na kuzuia upeo wake wa kuuona mpira pamoja na kupambana naye moja kwa moja kuupata mpira .

*Kujipatia faida kwa kuwa kwenye sehemu ya kuotea au off side kunamaanisha kuucheza mpira  ambao....

 Umedunda na kumfikia mchezaji toka kwenye mwamba au mchezaji ambaye yuko kwenye eneo la kuotea.

  Au kuucheza mpira ambao umebadilishwa mwelekeo yaani deflection au kuparazwa au ambao umeokolewa kwa kutemwa na golikipa au mpinzani wakati mpinzani mwingine akiwa kwenye eneo la kuotea .

Mchezaji aliyeko kwenye eneo la kuotea ambaye anapokea mpira kutoka kwa mpinzani ambaye anapiga mpira kuelekea nyuma yaani back pass ambayo sio jaribio la kuokoa mpira hahesabiwi kujipatia faida yaani gaining advantage.

Sababu za mabadiliko haya.

Maneno haya yanatoa mijadala mingi kwa kuwa yamekuwa na tafsiri nyingi na yanaonekana kuwa hayana ufasaha wa kutosha . Tafsiri hizi mpya zinaendana sanjari na nyakati halisi za kimchezo yaani actual in game situations na zitatoa mkanganyiko kwa kile ambacho watu wanadhani ni mpira uliodunda au rebound , mpira wa kuparazwa au deflection  na wakati ambapo mpira umeokolewa .


Maamuzi mengine ya IFAB 

1.GoalLine Technology ( kama ilivyotolewa na FIFA)

Iliamuliwa kuwa waandaaji wa mashindano wanapaswa kuamua juu ya matumizi ya GLT kwenye mashindano husika . Kulikuwa na makubaliano ya wote kuwa vifaa au nyenzo za GLT zinapatikana kwenye uwanja basi zitumike kwa kuwa hazileti faida kwa timu yoyote.


2.Waamuzi wasaidizi wa ziada. (Kama ilivyotolewa na FIFA)

Kama ilivyopitishwa kwenye mkutano wa mwaka wa kibiashara wa FIFA uliofanyika oktoba 2012 , taarifa hii mpya ya waamuzi wasaidizi wa ziada itaongezwa kwenye toleo jipya la sheria za mchezo la mwaka 2013/2014.

Utekelezwaji 

Maamuzi ya mkutano mkuu wa mwaka wa bodi ambao ulijadili mabadiliko ya sheria za mchezo yanayabana mashirikisho na vyama wanachama kutekeleza mabadiliko haya kuanzia julai mosi 2013 ,lakini mashirikisho na vyama wanachama ambao misimu yake haijaisha mpaka kufikia julai mosi wao wanaweza kuchelewesha utekelezwaji wa sheria hizi kwenye mashindano yake mpaka mwanzo wa msimu ujao.

No comments:

Post a Comment