Search This Blog

Thursday, January 31, 2013

MABAO 28 YATINGA KIMIANI MZUNGUKO WA PILI LIGI KUU - TEGETE, NGASSA NA MCHA VIALI WATISHA

JUMLA ya mabao 28 yamefungwa kwenye mechi tisa za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulianza kutimua vumbi lake Januari 26, mwaka huu.

Kwa idadi hiyo ni sawa na wastani wa kila mchezo yamefungwa mabao matatu kwa mechi hizo tisa iliyochezwa kwenye viwanja vya mikoa tofauti.

Nyota Mrisho Ngassa wa Simba, Jerry Tegete wa Yanga, Khamis Mcha 'Vialli' wa Azam FC na Paulo Nonga wa Oljoro JKT walizifungia timu zao mabao mawili kila mmoja kwenye ushindi wa mabao 3-1.

Kiungo mchezeshaji wa Simba, Ramadhan Chombo 'Redondo' ameandika rekodi ya kufunga bao la mapema zaidi.


Nyota huyo alipachika bao hilo katika dakika pili kwenye mchezo wa kukata utepe dhidi ya African Lyon uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda mabao 3-1.  

No comments:

Post a Comment