Search This Blog

Thursday, December 27, 2012

ASILIMIA 82 YA MASHABIKI WA MADRID WANATAKA MOURINHO ATIMULIWE KAZI REAL MADRID

Mashabiki wa Real Madrid wameamua. Wanataka Mourinho aondoke Bernabeu.

Kufuatia kupigwa benchi kwa Casillas katika mechi dhidi ya Malagamtandao wa gazeti maarufu nchini Hispania MARCA.com uliuliza "Je inabidi Real Madrid imtimue Mourinho?" na majibu ya takribani wasomaji 100,000 yalikuja yakisema ndio kwa asilimia  82.4%.

Kwa mujibu wa MARCA, mapenzi baina ya washabiki wa Los Blancos na Mourinho yamekwisha kabisa. Madrid wamekuwa na mfululizo wa matokeo mabaya katika kipindi cha hivi karibuni na kusababisha maneno mengi juu ya mustakabli wa kocha Jose Mourinho ndani ya klabu hiyo.

Real Madrid wapo nyuma kwa 16 dhidi ya viongozi wa La Liga Barcelona, na tayari Mourinho ameshasema kwamba ubingwa wa La liga msimu huu hawawezi kushinda tena, na inasemekana kwamba ikiwa atashindwa kuiongoza klabu hiyo kushinda ubingwa wa 10 wa mabingwa wa ulaya basi Mreno huyo atatemeshwa kibarua chake mwishoni mwa msimu.

5 comments:

  1. Morinho kufukuzwa Madrid halitokuwa jambo la kushtusha sana kwangu kwa sababu mbili,kwanza utamaduni wa Madrid wa kutokuwa na uvumilivu na makocha na kupelekea kuwatimua,lkini pili au kubwa zaidi Morinho sio aina ya mtanayefit falsafa za madrid au utamaduni wa soka wa Madrid,Morinho angefiti zaidi katika timu za ujerumani,england hasa Man united ambao hawahitaji vitu vingi zaidi ya vikombe na hata italy ambako alifanikiwa,lkn kwa spain hasa Madrid ambao wamezoea mpira wa akili zaidi,pasi nyingi na kuuchezea mpira zaidi huku wakitumia nguvu kidogo,kwa Morinho nahisi anateseka sana,.Kwa maana hiyo sito shangaa endapo atatupiwa virago Bernabeu..

    ReplyDelete
  2. Go back daddy to your lovely club Chelsea

    ReplyDelete
  3. ndo kazi yao ilivyo makocha, haina heshima hata kidogo, binafsi sijaona kibaya kwa mourinho, mimi nachoona jamaa anataka ndoo ya klabu BINGWA(UEFA) ndo malengo yake, kama kombe la nyumbani na mfalme ashawapatia, but mashabiki hawaoni hili. jose is best to me.

    ReplyDelete
  4. nadhani inabidi apewe mda zaidi, kwan msimu uliopita tu kawaletea mafanikio, najua isue inayosumbua ni kuachwa mbali na barca

    ReplyDelete
  5. Jose will remain the icon of achieved among coaches,amekuja madrid timu ikiwa imegeuzwa zulia la kukanyagia na barca but ameweza kuwafunga barca,kuchukua kombe la ligi na mfalme na pia kufika nusu fainali ya uefa ambapo timu ilikuwa ikiishia round ya pili,so jose anastahili heshima

    ReplyDelete