Search This Blog

Thursday, December 27, 2012

BRUNO GOMES MBRAZIL ANAYEKUJA OLD TRAFFORD MWAKANI - AIPA UBINGWA TIMU YAKE - ACHUKUA KIATU CHA DHAHABU

Mchezaji aliyesajiliwa na Manchester United kutoka Brazil Bruno Gomes ameiongoza klabu yake ya Desportivo Brasil kutwaa ubingwa nchini hiyo wa vijana wenye miaka U17. 

Gomes, 16, atajiunga na United kipindi kijacho kiangazi, alifunga hat trick katika fainali ya pili ya kugombea ubingwa huo dhidi  MarĂ­lia, na mwishowe Desportivo wakashinda 6-0

Mshambuliaji huyo hatari, tayari amekuwa chaguo muhimu katika kikosi cha Brazil cha vijana chini ya umri wa miaka 17, amefunga mabao 27 katika mechi 32 na kubeba kiatu cha dhahabu.

United wana mahusiano rasmi na klabu ya Desportivo Brasil, ambao wachezaji wao wamefunga mabao 88 katika mechi 32 msimu huu.

Inaeleweka kwamba pamoja na Gomes, United wapo katika mazungumzo ya kumsajili winga wa Desportivo aitwaye Welder.
Desportivo pia walishinda ubingwa Milk Cup huko Northern Ireland mwaka huu.

No comments:

Post a Comment