Search This Blog

Monday, December 24, 2012

KUELEKEA MATAIFA YA AFRIKA: SHOLA AMEOBI AKATAA KUICHEZEA NIGERIA - VICTOR MOSES ARUHUSIWA KUICHEZA SUPER EAGLES

Mshambuliaji wa Newcastle United Shola Ameobi amesema kuwa hatashiriki katika michuano ya kuwania Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika na timu ya taifa ya Nigeria.
Haya ni kwa mujibu wa kocha mkuu wa klabu hiyo Allan Pardew.
Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza ya vijana wasiozidi umri wa miaka 21, ametajwa katika kikosi kitakachoakilisha Nigeria katika fainali hizo zitakazo andaliwa nchini Afrika Kusini.
Kocha wa Nigeria Stephen Keshi amesema ana mataumaini makubwa kuwa mchezaji huyo atabadili uamuzi huo na kujiunga na timu hiyo kabla ya kuelekea nchini Afrika Kusini.
Lakini Pardew amesema mchezaji huyo mwenye umri wa maika 31, hataweza kushiriki katika fainali hizo za Afrika zitakazoanza tarehe kumi na tisa Januari.
Ameobi alizaliwa katika eneo la Zaria, Kaskazini mwa Nigeria kabla ya kuhamia Uingereza kuishi na wazazi wake akiwa na umri wa miaka mitano.

Chini ya sheria za FIFA wachezaji ambao wamewakilisha taifa moja katika mashindano ya vijana chipukizi anaweza kuichezea timu ya taifa lingine ikiwa atatimiza masharti yaliyowekwa
Ameobi alijumuishwa katika kikosi cha Super Eagles miaka kumi iliyopita lakini alikataa kujiunga nalo akisema nia yake ilikuwa ni kuichezea timu ya taifa ya Uingereza.
Mchezaji huyo hata hivyo alipewa kibali na shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA kuichezea taifa lake mwezi uliopita pamoja na mchezaji wa Chelsea Victor Moses.
Alicheza mechi yake ya kwanza na Super Eagles mwezi uliopita wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Venezuella ambapo Nigeria ilishinda kwa magoli matatu kwa moja.
Nigeria imo katika kundi la C na itacheza na mabingwa watetezi Zambia, Ethiopia na Burkina Faso katika mechi za raundi ya kwanza.

1 comment:

  1. Sitoshangaa endapo hatobadili msimamo wake kwa sababu,hakukulia ktk mazingira ya Nigeria,hafahamu watu wake wakoje,tamaduni zao hasa zikoje,hafahamu taifa linahitaji nini,zaidi ya kutamani kuchezea England kwa kuwa ndipo alipokulia,anafahamu kila kitu kuhusu England,hata kama atabadili uamuzi wake,naamini kujituma kwake,au ule uchungu wa kupigania taifa lake,utakuwa ni tofauti kabiasa na wachezaji wenzake ambao wanafahamu kila kitu kuhusu taifa lao..

    ReplyDelete