Search This Blog

Tuesday, December 25, 2012

KATONGO: SHOMARI KAPOMBE NI HATARI - AENDE AKACHEZE SOKA LA KULIPWA NJE

KIUNGO msumbufu wa Zambia, Felix Katongo, amemkubali sana  Shomari Kapombe wa Simba na Taifa Stars na amemshauri kusaka timu nje ya nchi.

Katongo alisema: "Nafikiri Tanzania (Taifa Stars) ilicheza vizuri. Lakini nilivutiwa zaidi na beki wa kushoto, (Shomari Kapombe)," alisema staa huyo anayekipiga na klabu ya Green Buffaloes.

Felix, ambaye kaka yake ni nahodha wa Zambia, Christopher Katongo aliongeza: "Nafikiri bado ni mchezaji mdogo. Pia, anatakiwa kujiendeleza kisoka kufikia malengo aliyojiwekea.

"Nilivutiwa zaidi na jinsi alivyokuwa akicheza hasa utulivu wake. Pia, kusaidia timu kushambulia, alitusumbua sana," alisisitiza.

Katongo ndio aliongoza kwa kupiga mashuti kwenye lango la Stars kama ilivyokuwa kwa Kapombe licha ya kucheza nafasi ya ulinzi. 


Source:Mwanaspoti

2 comments:

  1. KATONGO TUMEKUSIKIA LAKINI WACHEZAJI WETU NI WA HAPA HAPA TU YANGA VS SIMBA BASI HAWATAKI LENGINE AKIENDA KUCHEZA FC BASLE JANGWANI HAWATAMUONA NA KUMSIFIA KWA KUMPA ELFU KUMI BAADA YA MECHI

    ReplyDelete
  2. Najiuliza Hawa mawkala hapa kwetu wanafanya nini. Kipaji alichonacho Kapombe ni lulu inayopaswa kuchangamkiwa haraka sana. lakini nashangaa pado yupoyupo. huu ni wakati muafaka wa yeye kucheza nje, ikipita miaka mitatu tu, basi nae atakuwa wa HAPAHAPA. Amkeni wachezaji wa bongo.

    ReplyDelete