Search This Blog

Wednesday, December 26, 2012

NINI BALLON D'OR - RONALDO ATOSWA KATIKA TUZO ZA MASHABIKI WA MADRID - CASILLAS MCHEZAJI WAO BORA 2012

Hivi sasa inaonekna ni wazi Lionel Messi atatajwa kuwa mchezaji bora wa dunia mapema mwezi ujao, akimshinda mpinzani wake wa karibu Cristiano Ronaldo ambaye kwa sasa hakubaliki hata na mashabiki wa klabu yake ya Real Madrid.

Katika utafiti rasmi uliofanywa na taasisi moja huko jijni Madrid umeonyesha kwamba Nahodha wa timu hiyo Iker Cassilas na beki wa kulia Sergio Ramos ndio wachezaji bora wa klabu hiyo kwa mwaka huu wakifuatiwa na mreno Cristiano Ronaldo - kwa mujibu kura za washabiki 30,000.

Katika utafiti huo mashabiki wamewapa Wahispani Casillas na Ramos wastani wa 6.9 huku Ronaldo akiwafuatia kwa kupata wastani wa 6.6.

Hali hii inaonekana itazidi kumfanya Ronaldo kukosa furaha kama mwenyewe alivyosema huko nyuma, na kwa hakika itazidi kuongeza tetesi za mshambuliaji huyo kutaka kuondoka Santiago Bernabeu huku vilabu vya Man City, Man United na PSG wakiwa tayari na ndoano zao kumvua samaki wa gharama zaidi katika bahari ya soka.

1 comment:

  1. Kura walizopishana ni chache sana,na hii imechangiwa zaidi na sababu mbili,kwanza bifu la chinichini kati ya Iker na Ronaldo,pili Iker na Ramos ni vipenzi vya wahispania,lkn pia ikichagizwa na unahodha alionao Iker
    .Kifupi Wahispain wanathamini sana vyao na hata wachezaji wanaumoja sn,ndio maana hata Iker alisema wazi kabisa kuwa Iniesta ndiye bora na anastahili kuchukua tuzo ya uchezaji bora wa dunia,akijifanya hamuoni Messi..kwa hilo wahispaniola nawapongeza..

    ReplyDelete