Search This Blog

Wednesday, December 7, 2011

VIINGILIO VYA NUSU FAINALI YA CHALLENGE CUP.

NUSU FAINALI CECAFA TUSKER CHALLENGE

Mechi mbili za nusu fainali kuwania ubingwa wa 35 wa michuano ya CECAFA Tusker Challenge Cup inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) zinachezwa kesho (Desemba 8 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Nusu fainali ya kwanza itakayozikutanisha Rwanda na Sudan itachezwa kuanzia saa 8.00 mchana na kufuatiwa na ile ya pili kati ya mabingwa watetezi Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) na Uganda (The Cranes) itakayoanza saa 10.00 jioni.

Viingilio katika mechi hizo ni sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B, n ash. 20,000 kwa VIP A.

Mechi ya fainali na ya kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa Desemba 10 mwaka huu. Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) atapata dola za Marekani 30,000, makamu bingwa dola 20,000 na mshindi wa tatu dola 10,000.

No comments:

Post a Comment