Search This Blog

Saturday, December 10, 2011

UNITED KUWAKOSA WACHEZAJI 9 LEO DHIDI YA WOLVES


Manchester United imethibitisha kua beki wake Nemanja Vidic hawezi kuonekana tena uwanjani katika msimu mzima baada ya kuondolewa uwanjani kwa kutumia machela baada ya kuumia goti kwenye mechi na Basel ndani ya Ligi ya mabingwa.

kocha Ferguson amesikitika kwasababu alihisi jamaa angetibiwa na kuwa poa ndani ya kipindi kifupi, kumbe sivyo, ambapo nafasi yake inaweza kuchukuliwa na Jones au Smalling.

BBC wamesema Ferguson anakabiliwa na kigezo cha kupoteza hadi wachezaji tisa jumamosi hii wakati watakapocheza na Wolves, ambapo Miongoni mwa wachezaji wasioweza kumsaidia Ferguson ni Michael Owen, Anderson, Tom Cleverley, Fabio, Rafael na Javier Hernandez pamoja na mshambuliaji wa upande wa kushoto Ashley Young alionekana kuzidi kutonesha jeraha la kidole chake katika mechi dhidi ya Basel ambapo ilibidi aondolewe mapema kwenye kipindi cha pili.

MillardAyo.com

No comments:

Post a Comment