Search This Blog

Thursday, December 8, 2011

ROONEY APOOZWA MACHUNGU: APUNGUZIWA ADHABU YA KUFUNGIWA NA UEFA


Mshambuliaji wa England na Manchester United Wayne Rooney leo amepunguziwa na UEFA kifungo chake cha mechi 3 na sasa atatumukia kifungo cha mechi mbili tu kufuatia rufaa yake iliyosikilizwa hivi leo huko Nyon, Uswisi huku mwenyewe akihudhuria.
Rooney, Miaka 26, alifungiwa mechi 3 na UEFA baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumpiga teke Beki wa Montenegro Miodrag Dzudovic England ilipocheza na nchi hiyo mwezi Oktoba na kutoka sare 2-2 na kufuzu kuingia Fainali za EURO 2012 zitakazochezwa Juni Mwakani huko Nchini Poland na Ukraine.
Kupunguziwa kwa adhabu hiyo kutamfanya Rooney aweze kucheza mechi ya mwisho ya Kundi D dhidi ya wenyeji Ukraine hapo Juni 19 na kuzikosa mechi mbili za kwanza dhidi ya France na Sweden,
MECHI ZA ENGLAND Kundi D EURO 2012:
Continue reading the main story
11 Juni - France (Donetsk)
15 Juni - Sweden (Kiev)
19 Juni - Ukraine (Donetsk)
Msemaji wa UEFA amesema adhabu ya kufungiwa kwa mechi ya 3 imesimamishwa kwa Miaka minne kuangalia mwenendo wake na itarudi ikiwa tu atafanya kosa kama hilo tena kwenye michuano ya UEFA inayohusisha Timu ya Taifa tu.
Pamoja na kusimamishwa adhabu hiyo Rooney itabidi atumikie kazi ya kijamii kwa Siku nzima kwenye miradi ya UEFA.
Rufaa ya Rooney ilisikilizwa na Jopo la Watu watatu na ilichukua muda wa Saa moja na Nusu huku Rooney akiwa pamoja na Kocha wa England Fabio Capello na Mawakili wao.

No comments:

Post a Comment