Search This Blog

Tuesday, December 6, 2011

LUIS SUAREZ MATATANI TENA - ANGALIA ALICHOFANYA.


Akiwa bado na kesi ya kumtolea maneno ya kibaguzi Patrice Evra, mchezaji wa Liverpool Luis Suarez anaweza kujikuta yupo kwenye matatizo zaidi baada ya kuwaonyeshea ishara ya kidole cha kati mashabiki wa Fulham baada ya mchezo uliozikutanisha timu zao katika muendelezo wa ligi kuu ya England usiku wa jana.

Suarez jana alikuwa katika wakati mgumu baada ya mashabiki wa Fulham katika uwanja wa Craven Cottage walipokuwa wakimzomea kwa kumuita “mdanganyifu” kutokana na kitendo chake cha kujiangusha katika mechi hiyo.

Kutokana na kitendo alichofanya Suarez ambacho mara nyingi hutatafsiriwa kuwa ni tusi, then anaweza akajikuta katika balaa la kukumbana na adhabu kutoka FA, ikiwa kamati ya nidhamu itaona ana makosa pindi watakapokaa kumjadili leo Jumanne.

No comments:

Post a Comment