Search This Blog

Wednesday, December 7, 2011

Mc​hezaji wa zamani wa Prisiner MADESHO MOYE amefariki dunia katika hospitali ya KCMC

Na Dixon Busagaga,Moshi.

TASNIA ya mchezo wa soka nchini imepata pigo kufuatia kifo cha
mchezaji wa zamani wa timu ya soka ya Prisiner Madesho Moye
kilichotokea leo majira ya saa nne asubuhi katika hospitali ya rufaa
ya KCMC.

Madesho aliyekuwa Rais wa timu ya soka ya Moshi Veterani aliugua
ghafla juzi muda mchache baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki
kati ya timu yake ya Moshi veterani na timu ya Wazee kutoka mkoani
Arusha ambayo alicheza kwa muda wote wa mchezo.

Taarifa za awali zilisema kuwa mara baada ya mchezo kumalizika
kulifanyika sherehe ndogo ya kupongezana kwa timu hizo mbili ambapo
mara baada ya sherehe hiyo kwisha Madesho alipanda gari yake na
kuelekea nyumbani ndipo hali ilibadilika ghafla na kusadiwa na
wachezaji waliokuwepo uwanjani hapo.

Baadae Madesho alikimbizwa katika hospitali ya Kilimanjaro hali
ilivyozidi kuwa mbaya alihamishiwa katika hospitali ya rufaa ya Kcmc
ambako alipokelewa na kulazwa katika chumba cha uangalizi kwa wagonjwa
mahututi(ICU) ndipo hado kufikia leo saa 4 asubuhi taarifa za kifo
chake ndipo zilipotangazwa.

Marehemu Madesho aliwahi kuzichezea timu za Prisner,Boma Fc,Kiboko
Msheli na timu nyingine nyingi kabla ya kuamua kustaafu na kuendelea
na kazi aliyokuwa akifanya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)katika mkoa
wa Kilimanjaro.

MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI ,AMEEN.

Madesho Moye akiwa amebeba kombe baada ya kufanikiwa kushinda kikombe
hicho katika mashindano ya Pasaka ambayo huandaliwa kila mwaka na
mamlaka ya bandali ya nchini Kenya.

Madesho Moye wa pili kutoka kulia (waliopiga magoti)akiwa na kikosi
cha timu ya soka ya Moshi veterani ya mkoani Kilimanjaro kilipofanya
ziara nchini Kenya April Mwaka huu katika mashindano ya kombe la
Pasaka ambalo timu hiyo ilifanikiwa kunyakua.



Madesho Moye akiwa katika picha ya pamoja na mchezaji wa timu ya soka
ya Standard Chartered ya jijini Nairobi ambaye jina lake
halikufahamika mara moja mara baada ya mchezo wa fainali uliopigwa
katika uwanja wa KPA mwaka huu.



Madesho Moye akiwa amebeba kikombe mara baada ya kukabidhiwa baada ya
kuwa washindi katika mashindano ya Pasaka yaliyofanyika nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment