Search This Blog

Monday, August 5, 2013

EXCLUSIVE: MWINYI KAZIMOTO AKIWA NA RAUL GONZALEZ BLANCO MAZOEZINI QATAR - AONGEA RASMI KUHUSU HATMA YAKE

Kiungo wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba Mwinyi Kazimoto akiwa na Gwiji wa soka wa Hispania na Real Madrid Raul Gonzalez huko Qatar alipokuwa ameenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa. Mtandao huu umepata nafasi ya kuongea na Kazimoto na kwa kifupi ameomba radhi kwa kutoroka - pia amesema amefanikiwa kupata timu huko alipo. Je ungependa kujua Simba imelipwa shilingi ngapi kwenye uhamisho huu wa Kazimoto???? - Endelea kutembelea mtandao huu.



2 comments:

  1. Shaffih niliwasikiliza kwenye Sports bar mkizungumza na Kazimoto; kiukweli nakupongeza kwa jitihada zako za kumtafuta Mwinyi mpaka kufanyanae mahojiano. Kitu ambacho sikubaliani na wewe ni jinsi unavyozungumzia transferring of funds kwa wachezaji wa Simba wanavyouzwa na fedha kuingia kwenye mifuko ya wajanja.

    JEFF aliongelea kidogo kuhusu justification ya wajanja hao wanaochukua fedha hizo, lakini hakufunguka vya kutosha. Mimi nadhani kama kweli tunapenda kufuata taratibu basi tungeanza kuiuliza kwa mfano Timu ya Simba ililipa kiasi gani kutoka kwenye account yake kununua wachezaji kama OKWI, OCHAN, SAMATTA, MRWANDA, HENRY JOSEPH, SUNZU na wengine, tukishajua account ya club ilitumika kununua wachezaji hao ndipo tutakuwa na haki(wanasheria wanaita locus stand)ya kujua na kudai malipo ya wachezaji hao pamoja na ya Kazimoto pindi wanapouzwa yaingie account ya SIMBA.

    Tofauti na a hapo Account ya Club ya Simba haina chake. Kuendelea kuhoji ni sawasawa na BABA ambaye hukumsomesha mtoto, mtoto huyo kasomeshwa na wasamaliawema then baba unakuja kudai mshahara wa mwanao baada ya mtoto kupata kazi. It cant be done.

    ReplyDelete
  2. PHILUSUPHY KAZIMOTO jamaa mbaya kama mbwiga ila ndy hvy kibongobongo muda mwingine inabidi ujilipue liwalo na liwe angesubiri mpk azeeke.

    ReplyDelete