Search This Blog

Friday, August 9, 2013

JOSE MOURINHO: "HATUTOKATA TAMAA KATIKA MPANGO WA KUMSAJILI ROONEY - TUTAFANYA KILA NJIA KUMLETA STAMFORD BRIDGE"


Jose Mourinho amesisitiza kwamba atapigana mpaka siku ya mwisho katika jaribio lake la kumsaini Wayne Rooney.
Chelsea tayari walishatuma ofa mbili ambazo zimekataliwa na  Manchester United, ofa ya mwisho inayotajwa kuwa ni zaidi ya paundi million 25 ilitumwa jumapili. Lakini Mourinho alisema: "Hatuna kizuizi cha muda kwenye suala hili. 

‘Tumemuona Rooney kama ni mchezaji ambaye tungependa kuwa nae. Tumefanya kila kitu katika utaratibu unaopaswa na tutafanya hivyo mpaka siku ya mwisho ya usajili. Tunafnya kila kitu tukizingatia sheria, kutoa ofa rasmi kwa klabu moja kwa moja.
‘Hakujawahi kuwepo kwa mawasiliano na mchezaji, hakijatokea kitu kama hicho. Tusubiri tuone kama mambo yatabadilika.’ 
Rooney inaaminika kwamba amemwambia kocha wake David Moyes kwamba anataka kuondoka, lakini United imekuwa ikisisitiza kwamba hauzwi. 

No comments:

Post a Comment