Search This Blog

Friday, August 9, 2013

MMILIKI WA LIVERPOOL ASEMA "KUWAUZIA SUAREZ ARSENAL UTAKUWA NI UPUMBAVU - HAENDI POPOTE DIRISHA HILI LA USAJILI."


Luis Suarez amezidi kupata vizingiti vikubwa katika harakati zake za kutaka kuhama Liverpool, baada ya kuambiwa na mmiliki wa Liverpool John Henry warning: “Huendi popote”.

Mmiliki huyo wa Liverpool amesema kwamba ni upumbuvu kuanza hata kufikiri kufanya biashara na Arsena ya mshambuliaji huyo wa Uruguay.
Na mmarekani huyo amesema kwamba kitendo alichokifanya Suarez kilivuka mipaka, huku akisisitiza kwamba mshambuliaji huyo hatouzwa kwenda klabu yoyote mpaka dirisha la usajili litakapofungwa September 2 - pia akisema uamuzi wa kutokumuuza Surez hautokani na masuala ya fedha. Henry alisema: “Hatuwezi kumuuza Luis. Ni kwa sababu za kisoka kabisa, na sio masuala ya fedha.

“Hii ni kwasababu mpaka sasa ni vigumu kupata mchezaji wa kuziba pengo lake kwa maana wachezaji wazuri wote wameshahama. Hivyo ni sababu za kisoka, hatuwezi kumuuza - hasa kwa klabu ya Arsenal.

“Kuwauzia mahasimu wetu mchezaji huyu utakuwa ni upumbavu kabisa."

No comments:

Post a Comment