Search This Blog

Thursday, August 8, 2013

CRISTIANO RONALDO AITUNGUA CHELSEA MABAO MAWILI NA KUMWAMBIA MOURINHO - "NAPENDELEA KUZUNGUMZA KUPITIA MATENDO YANGU YA UWANJANI"

Cristiano Ronaldo alikuwa na sababu nyingi zaidi ya kushangilia goli lake katika mechi ya pre-season - na kumuonyesha boss wa Chelsea Jose Mourinho aliyemdhiaki kabla ya mchezo kwamba yeye ni "Ronaldo" wa aina gani.

Ronaldo alifunga mabao mawili na kuiwezesha Real Madrid kuifunga 3-1 Chelsea katika Guinness International Champions Cup jijini Miami.

Baada ya goli lake la kwanza alilofunga kwa mkwaju wa faulo, hakushangilia bali aligeuka mbele ya jukwaa la mashabiki na kuonyesha kifua chake huku akitikisa kichwa.
 Baada ya mchezo huo Ronaldo alizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maneno ya maneno Mourinho kwamba Ronaldo orijino ni yule wa Brazil - Cristiano alisema: "Napendelea kuzungumza kwa vitendo vyangu vya uwanjani na sio mara pengine popote"


1 comment:

  1. Huyo ndo CR7 bhana,As i said lazima atascore,RIP MOURINHO & CHELSEA

    ReplyDelete