Search This Blog

Saturday, August 10, 2013

OFFICIAL: GERVINHO AHAMA ARSENAL BAADA YA MISIMU MIWILI - AS ROMA YAMNYAKUA KWA £8M


Usajili wa wachezaji mbalimbali unazidi kushika kasi barani ulaya.

Winga Mshambuliaji wa Ivory Coast, Gervais Lombe Yao Kouassi maarufu kama Gervinho amekamilisha uhamisho wa kuichezea As Roma ya Italia.

Gervinho alihamia Arsenal mwaka 2011 akitokea Lile ya Ufaransa. Uhamisho huo wa Gervinho umetajwa kuwa wa pound milioni 8 walizopewa Arsenal.

Msimu wake wa kwanza aliifungia Arsenal magoli manne kabla ya kufunga magoli saba msimu uliopita.

Amekuwa akipata ushindani wa kuwemo kwenye kikosi cha kwanza cha Arsene Wenger, na huenda usajili wake wa kuhamia Seria A utakuwa changamoto mpya kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.

1 comment: