Search This Blog

Tuesday, August 6, 2013

EXCLUSIVE: MWINYI KAZIMOTO: "NIMEILIPA SIMBA $40,000 ILI NICHEZE SOKA QATAR - NAOMBENI MSAMAHA KWA KUTOROKA"

Wiki kadhaa baada ya kutoroka nchini na kukimbilia nchini Qatar kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio ya soka la kulipwa, leo hii kiungo wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba Mwinyi Kazimoto amezungumza rasmi na mtandao huu na kutoa taarifa nzima ya kuhusu sakata lake la kutoroka.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Doha Qatar na Shaffih Dauda, Mwinyi Kazimoto kwanza amekiri kwamba alitoroka kwenda Qatar kwa nia ya kwenda kufanya majaribio, "Safari yangu ya kuja huku Qatar ilibidi iwe kabla hata sijacheza mechi ya marudiano na Ivory Coast, lakini kwa sababu nilikuwa na majukumu nilivumilia nikabaki mpaka nilipocheza mchezo wa kwanza dhidi ya Uganda, wakati tukiwa kambini kwa ajili ya mchezo wa pili ikabidi niondoke kwa sababu siku zilikuwa zinaenda na muda wangu wa kufanya majaribio ukawa unaisha," anazungumza Kazimoto

Alipoulizwa kama tayari ameshafuzu majaribio aliyoenda kufanya kiungo huyo wa zamani wa JKT Ruvu alisema: "Mwanzoni nilipata vilabu viwili vinavyoshiriki ligi daraja la kwanza ya huku, lakini nikachelewa majaribio na hivyo nikakosa nafasi. Baada ya hapo ndipo ikajitokeza timu ya Al-Markhiya Sports Club - inayoshiriki ligi ya daraja la pili na ikavutiwa nami na ikafanya mipango ya kunisajili."

Taarifa nchini zimeenea kwamba klabu ya Simba imepokea kiasi cha $35,000 kwa ajili ya kumuuza kiungo huyo, Je Kazimoto anasemaje juu ya hili? "Ni kweli kutokana na kwamba nilikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na Simba ilibidi nitoe kiasi cha fedha ($40,000 na sio $35,000 kama inavyoripotiwa) kutoka kwenye ada ya usajili wangu kuununua mkataba wangu uliobakia na Simba.


"Sasa hivi nimefanikiwa tayari kupata timu hii lakini ndoto yangu ni kujitahidi na kuweza kucheza ligi ya juu kabisa hapa. Vilevile ningependa kuwaomba radhi watanzania wote na klabu yangu ya Simba kwa kitendo cha kutoroka wakati nikiwa nahitajika. Nafasi ya kucheza soka la kulipwa ilikuwa ni muhimu kwa maisha yangu na sikutaka niipoteze hivyo naomba wanielewe na kunisamehe."



10 comments:

  1. Tumekusamehe kazimoto ukizingatia mpira ndio elimu yako na umri unaenda na pia bora ulivyoamua kiume cos kibongo bongo yangekutokea ya kaseja kila la kheri mwenyezi mungu akuongoze na utimize ndoto zako wenzetu wa west ghana,nigeria etc wanafanya kama ulivyofanya ww na wala sio zambi mtu kutafuta maisha,Tff tunawaomba wakusamehe ukizingatia umeenda kufungua milango kwa watanzania wenzio

    ReplyDelete
  2. kaza buti soka halina muhamara mek money ukiwa na nguvu baadae upumzike mr ball dancer xema ni vyema ulivyoomba taifa msamaha na klabu yako

    ReplyDelete
  3. Big up ball dancer Mwinyi Kazimoto;kila la kheri TFF waache hazira wao wanafanya utumbo mara ngapi lakini watanzania tunawasamehe.

    ReplyDelete
  4. nia yako siyo mbaya kaka naamini wote wamekuelewa nimependa umejinyenyekeza na kuomba radhi kama kuna mtu atakuwa na kinyonggo juu ya hilo, naamin atakuwa hapendi maendeleo yako nakutakia mafanikio mema. MUNGU akubariki kaka

    ReplyDelete
  5. upo sawa kijana,we endelea na kutafuta maisha,soka la bongo waachie wendawazimu wasiotaka watu wafanikiwe...

    ReplyDelete
  6. una aja ya kuomba msamaa mwinyi ile ni swla zuli ulilo liamua kwa ajiri ya maisha yako ya badae hapa haƶmna soka ni mazoezi tu hapa bongo cheza mpila huko ndio kuna mpila kaza sifa usibweteke nazo inchi nzuri sana hiyo kaka me nimeish kama ulaya! Usiadaike na kuja kutesa bongo maisha ya huku yatakuwa yale yale piga soka njooo ujiemdeleze huku kima isha mollah wawe p1 nmawe

    ReplyDelete
  7. Mimi niliposikia tu Mwinyi kaondoka kwenda Qatar niliona alifanya la maana, nikawa nawashangaa Simba na TFF kusema tutahakikisha hachezi soka!!! hawa ni watu wa ajabu sana mchezaji yuko kiwango mpaka anatamaniwa na nchi za kigeni, wabongo wanataka kumbania. Mwacheni afaidike na kipaji na ujuzi wake aliojaaliwa. Mbona wataalamu na madaktari Watanzania wanakimbilia nje bila kuaga pamoja na kwamba wamesomeshwa kwa pesa za Tanzania?

    ReplyDelete
  8. Pamoja sana kazimoto komaa tu huko mpira wa bongo waachie wakina rage na siasa zao..

    ReplyDelete
  9. Mbele mbele tu, we jiendee kwa amani bana.

    ReplyDelete