Search This Blog

Friday, June 3, 2011

SAJILINI MAJINA MAKUBWA AU NAONDOKA


LUKA MODRIC ameiambia klabu yake ya Tottenham kusajili wachezaji wazuri na wakubwa ama atafungasha virago vyake na kuondoka.

The Croatian midfielder mwenye thamani ya paundi million 25 anasakwa kwa udi na uvumba na klabu za Manchester United na matajiri wa Eastlands the mega-rich Manchester City.

Modric, 25, alisaini mkataba wa miaka 6 msimu uliopita anansisitiza ana furaha kuwa kwenye kikosi cha Harry Redknapp lakini ana wasiwasi na mwenendo wa klabu msimu ujao.

Mtu wa ndani wa Spurs anasema Harry hataki kumuuza Modric lakini Luka mwenyewe ana ndoto za kupata mafanikio makubwa zaidi.

"Modric anasubiri kuona kama Redknapp atasajili wachezaji ambao ni wakubwa halafu ndio atajua nini hatma yake ndani klabu hii".

Wakati huo huo Roman Pavlychenko amesema yupo tayari kuendelea kubaki White Hart Lane, "Nia yangu ni kubaki hapa na kupata mafanikio makubwa, baada ya mapumziko nitarudi kujadili mkataba mpya.

No comments:

Post a Comment