Search This Blog

Friday, June 3, 2011

FABREGAS NI WENU KWA PAUNDI MILLION 54- ARSENAL WAIAMBIA REAL


ARSENAL wameiambia Real Madrid kuwa bei ya kumuuza Cesc Fabregas inaanzia paundi millioni 54.

Director wa Real, Jose Angel Sanchez aliwasiliana na Arsenal saa moja baada ya Wenger kukiri kuwa hakujakuwa na timu yoyote iliowasilisha maombi ya kumtaka Fabregas, na Spanish giants sasa wapo tayari kukubaliana na Gunners na kuwapiku mahasimu wao wakubwa Barcelona.

Chanzo cha habari kutoka Madrid kilisema: Raisi Florentino Perez amesema kuwa Fabregas ni moja ya usajili mzuri na zaidi utawaumiza sana Barca.Anaamini kumsajili Cesc itakuwa ni jambo la maana msimu ujao na atafanya chochote kinachohitajika kuwapiku Barca next season.

Perz yupo tayari kuidhinisha matumizi ya £100m kwa kumpata Fabregas na mshambuliaji wa Atletico Madrid anayewania pia na Barca na Man City Sergio "Kun" Aguero.
Real sources wanadai kuwa Arsenal wameweka wazi kabisa kuwa hatamuuza Cesc kwa timu yoyote ya Uingereza.

Barcelona-born midfielder Fabregas, 24, mwaka jana aliweka wazi nia yake ya kutaka kurudi Nou Camp baada ya kukaa England kwa miaka 8, lakini newly-crowned European Champions hawapo tayari kuongeza dau la £30million ambalo lilikataliwa na Arsenal msimu uliopita

No comments:

Post a Comment