Search This Blog

Wednesday, June 1, 2011

DE GEA, THE NEW VAN DER SAR OR THE NEW TAIBI

Kwa Manager ambaye ana rekodi ya kununua na kugundua vipaji vya wachezaji wakubwa kwa takribani robo karne, Sir Alex Ferguson's record linapokuja suala goalkeeper huwa anapata wakati mgumu kidogo.
Baada ya kuondoka kwa moja ya magolikipa bora kabisa kuwahi kutokea katika historia ya Man United, Peter Schmeichel mwaka 1999 ilimchukua miaka zaidi ya sita Ferguson kupata mbadala sahihi wa kipa huyo raia ya Denmark pale ambapo alikuja kumsajili Edwin Van Der Sar kutoka Fulham kwa paundi millioni 2.
Mark Bosnich, Paul Rachubka, Massimo Taibi, Fabien Barthez, Raimond van der Gouw, Andy Goram, Roy Carroll, Tim Howard, Ricardo and Nick Culkin wote walijaribu kuvaa gloves za Schmeichel lakini hazikuwatosha mpaka alipowasili Van Der Sar.
Sasa miaka 6 ya kuitumikia United kwa Van Der Sar imefikia ukingoni baada ya Mdachi huyo mwenye umri wa miaka 40 kuamua kutundika daluga na sasa Sir Alex Ferguson yupo katika mtihani mwingine wa kumtafuta mrithi sahihi wa mlinda mlango huyo ambaye ameichezea kwa mafanikio makubwa United.

Majina kadhaa yametajwa kumrithi Van Der Sar kuanzia Manuel Neurer, Marteen Stakelenburg, Hugo Lloris na David De Gea lakini hivi karibuni Sir Alex Ferguson ambaye amesema hataki kurudia makosa aliyoyafanya kipindi alipostaafu Schmeichel amemtaja David De Gea kuwa ndio mrithi sahihi wa Van Der Sar.

David De Gea ni moja ya magoli kipa bora kabisa katika ulimwengu wa soka kwa kipindi, ni raia wa Spain na anaichezea Atletico Madrid inayoshiriki La Liga., ana umri wa miaka 20.

Scouting team ya United inayoundwa na Jim Lawlor, Martin Ferguson(Mdogo wake Fergie), kocha wa magolikipa Eric Steele na Les Kershaw wamemthibitisha Da Gea Kuwa anafaa kuwa anafaa kumrithi Mdachi Van Der Sar.

Swali linaulizwa na wachambuzi wa soka duniani ni kwamba, pamoja na talent na potential aliyonayo Da Gea, je atakuwa mbadala sahihi wa Van Der Sar au atakuwa Massimo Taibi mpya, golikipa ambaye alifanya madudu makubwa aliposajiliwa kama mrithi wa Schmeichel.

Ferguson huwa na kawaida ya kuamini kuwa magolikipa wazuri ni ambao wana umri mkubwa, akisema ubora wao unazidi kuongezeka wanapofikia miaka ya 30 na kuendelea.Je golikipa kama Da Gea ambaye ameanza rasmi kucheza mashindano ya maana mwaka 2009 atakuwa na experience ya kutosha kuweza kulinda vizuri milingoti mitatu ya Old Trafford?

Mbadala wa Fabian Barthez, Tim Howard alisajiliwa akiwa miaka 24 na akafanikiwa kupata nafasi kikosi cha kwanza lakini akaishia kuisababisha United kupoteza mchezo dhidi ya FC porto katika robo fainali ya Champions League in 2004, na sasa ameamia Everton akiwa na miaka 32 kipaji chake kimeanza kuongezeka na kuzidi kuipa nguvu hoja ya Ferguson kuwa golikipa anakuwa bora kadri umri unavyokwenda.

Kwa upande wa Joe Hart mwenye umri wa miaka 24 amei-prove wrong falsafa ya Fergie kwa kuwa msimu bora kabisa akiwa na Manchester City baada ya kulinda vizuri milingoti ya Eastlands na kumuweka benchi Shay Given mwenye miaka 35, huku akifanikiwa kujipatia nafasi katika kikosi cha England chini ya Fabio Capello

De Gea is a superb shot-stopper, ana kipaji kikubwa na rekodi nzuri akiwa na Atletico na timu ya taifa ya Spain under 20, lakini anakosa experience na pia umri wake unapingana na falsafa ya Fergie kuhusu umri wa magolikipa bora.

Ukweli utathibitika kama De Gea ataweza ku-handle pressure ya kuichezea timu inayotajwa kuwa kubwa kuliko zote ulimwenguni., kama ataweza kufuata nyayo za Schmeichel na Van Der Sar na kuwa moja ya United Legend au atakuja kuwa kama Massimo Taibi

I



No comments:

Post a Comment