Search This Blog

Wednesday, June 1, 2011

OFFICIAL: BIG SAM KOCHA MPYA WA WEST HAM


Kocha wa zamani wa klabu ya Bolton na Blackburn Sam Allardyce jana usiku amesaini mkataba wa miaka 2 wenye thamani ya paundi millioni 3 wa kuifundisha West Ham, ambayo imeshuka daraja msimu huu.

Allardayce ambaye amekuwa nje ya soka tangu alipofukuzwa kazi na Blackburn atakuwa ndio the highest paid boss katika ligi ya daraja la kwanza, na akifanikiwa kuirudisha the Hammers in Premier League atapata bonus ya paundi million 1.25.

Big Sam anategemea kutambulishwa rasmi wiki ijayo na ataanza kazi haraka ya kukijenga kikosi ambacho kitakuwa na uwezo wa kupambana kuirudisha timu hiyo in EPL.

Wamiliki wa West Ham David Sullivan, David Gold na Karren Brady wamemwakikishia Big Sam budget nzuri ingawa kuna wachezaji itabidi wauzwe ili waweze kui-boost mkwanja wa kununulia wachezaji wengine,.

Wachezaji wanaotajwa kuuzwa na pamoja na Robert Green, Scott Parker and Calton Cole ambao kwa pamoja wanaweza kuiingizia klabu paundi millioni 18 ambazo zitatumika katika kununulia wachezaji wengine ambao watapambana ili kuwarudisha wagonga nyundo hao London katika ligi ya England.


No comments:

Post a Comment