Search This Blog

Saturday, June 4, 2011

ENGLAND YATOKA SARE NA USWISI NA LAMPARD AVUNJA REKODI


Timu ya taifa ya England imetoka sare na Uswisi katika michuano ya kugombea kucheza fainali za kombe la mataifa ya ulaya zitakozofanyika mwakani nchini Ukraine huku kiungo Frank Lampard akivunja rekodi kwa kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi kupitia mikwaju ya penalti akiwapita Alan Shearer na Rob Fowler.

Lampard ambaye alianza kuichezea England in October 10, 1999 dhidi ya Belgium akiwa na miaka 21 na siku 111, mpaka sasa ameshaitumikia Three Lions katika mechi 86, kati ya hizo 36 ni za kirafiki, kufuzu World Cup 20, World Cup finals 9, kufuzu EURO 15, EURO finals 4, michuano mingine 2.Amefunga magoli 22, 7 KATI YA HAYO AMETUPIA NYAVUNI KUPITIA MIKWAJU YA PENATI.

Amecheza jumla ya dakika 6385, amepata kadi 3 za njano, hajawahi kupata red card, goli lake la kwanza alifunga dhidi ya Croatia, amewahi kuwa kapteni mara 1 katika mechi dhidi ya Denmark.


No comments:

Post a Comment