Mshambuliaji wa Barca na Spain ametaja kikosi chake bora ambacho kinaundwa na wachezaji ambao amewahi kucheza nao timu moja na wale ambao amewahi kucheza dhidi yao, lakini cha ajabu na yeye mwenyewe amejiweka ndani ya kikosi hicho.
Goalkeeper Iker Casillas: Hakuna kusita linapokuja suala la kutaja jina la kwanza katika kikosi cha wachezaji ambao nimecheza nao timu moja au kupambana nao.Kwangu Iker Casillas ni golikipa bora duniani.Nimecheza nae timu moja, nimecheza dhidi yake na nimemshafunga lakini ni vigumu sana kumtungua.
Right-back Daniel Alves: Alves amekuwa na kipindi kizuri sana na nafikiri ndio beki wa kulia muhimu kuliko wote katika ligi ya Hispania, na sio kwamba ni beki tu yupo sehemu zote za uwanja.Watu wengine wanamzungumzia sasa kipindi yupo hapa Barca na wengine wanashangazwa na uwezo wake lakini alikuwa bora tangu kipindi yupo Sevilla.
Centre-back Rio Ferdinand Manchester [United] na Barcelona ndio bora ulaya kwa sasa, na Ferdinand ni kiongozi mzuri na beki bora, namkubali sana.Nimecheza dhidi yake kabla ya fainali ya Champions League, ana nguvu na anazuia vizuri.Nilifunga dhidi ya Manchester lakini haikuwa kazi rahisi na nilip[ofunga dhidi ya England yeye akiwa hacheza na nikagundua tofauti.
Centre-back Pepe: Pepe yupo vizuri mno na ni vigumu sana kucheza dhidi yake, ndio beki wa wakati ambaye nilihangaika mno kucheza dhidi yake.Ni mwepesi na nguvu sana.
Left-back Paolo Maldini Watu wengi huwa wanamchagua Paolo Maldini na mimi nakubaliana nao.Amefanya kila kitu katika kipindi chake cha uchezaji, ni moja ya wachezaji wazuri katika historia ya soka na anawakilisha kila kitu kizuri katika soka.
Midfielder Xavi: Ni raha sana kucheza na mtu ambaye anajua kucheza soka la kiufundi kama Xavi.Alikuwa ndio mchezaji bora wa EURO 2008, tulipochukua kombe hilo, ndio mtu anayeifanya Barcelona kuwa timu bora kwa sasa.Hapotezi mpira ni mfano bora ambao wote tunapaswa kuufuata.
Midfielder Andres Iniesta Kwa pamoja na Xavi, Iniesta ni wauaji.Wanafanya mambo yao vizuri na kwenye timu ukiwa na wale jamaa wawili katikati ya uwanja hakuna kitachoharibika.Huwezi kuwatenganisha Iniesta na Xavi kwasababu mchezo wao unaenda pamoja.Hawa ndio pea ya viungo bora ambao nimewahi kuwaona kwenye soka.
Midfielder Steven Gerrard Namkubali na kumpenda sana Steven Gerrard. Ni mtu ambaye namkubali kiukweli.Ana kila kitu kama kiungo.Napenda jinsi anavyocheza, ni kiongozi mzuri sana uwanjani, anafunga magoli, anapiga pasi nzuri, anakimbia vizuri, anakaba na ana nguvu sana.Kwa kifupi Gerro ni mchezaji aliyekamilika.
Striker Lionel Messi: Kuchagua watu mbele ni rahisi, Leo Messi upande mmoja na Cristiano Ronaldo upande mwingine.Nachagua formation ya 4-3-3 na nafikiri hakuna wa kubisha kuhusu watu hawa wawili kwa sababu ndio wachezaji bora kabisa kwa sasa duniani.Cristiano ni mchezaj mzuri lakini nitamchagua Messi kama mchezaji bora wa dunia kwa sababu vitu anavyofanya sijawahi ushuhudia katika ulimwengu wa soka.
Striker Cristiano Ronaldo Pamoja na Messi wanaweza kusababisha maafa kwa timu pinzani.Cristiano ana nguvu sana na uwezo mkubwa sana wa kucheza mipira ya faulo, anafunga kwa mashuti ya mbali na hata vichwa kwa kifupi anatisha.Vitu alivyovifanya akiwa na Manchester vinampa nafasi ya kuwa bora na sasa akiwa Real Madridi anaonyesha bado hamu ya ushindi.
Striker David Villa: Sasa mshambuliaji wa katikati, nani nimchague? aaaaaaa labda mimi, nimewahi kuwa mfungaji bora wa EURO, nafikiri ni kigezo kizuri.Siwezi kujenga kikosi kizuri kama hiki halafu mimi nisiwemo.Nafikiria nafasi za kufunga nitakazozipata nikicheza mbele ya Xavi, Iniesta, Gerrard, Messi na Ronaldo.
No comments:
Post a Comment