Search This Blog

Friday, June 3, 2011

NATAKA NIKUMBUKWE KAMA PELE NA MARADONA - RONALDO



Mfungaji bora La Liga amesema ana matamanio na ndoto za kuwa katika level za Maradona na Pele, soma mahojiano yake aliyoyafanya na mtandao mmoja wa intaneti kuzungumzia ndoto zake.

Ni miaka miwili tangu ujiunge na Real Madrid, vipi unayafurahia maisha ya hapa? Nafurahia sana kuwa hapa , klabu ni nzuri sana na nilitegemea hili.Miundombinu , washabiki na uwanja uzuri wake hauwelezeki.

Unajisikiaje kucheza na mtu kama Kaka ndani ya Real Madrid? Ukiwa unacheza timu moja na wachezaji wazuri inakuwa rahisi zaidi na Kaka ni mmojawapo, nafurahia sana kucheza pamoja nae.

Unayatizama vipi mafanikio yako ndani ya kikosi cha Manchester United? Nafikiri nilifanya kila kitu nilichotaka nikiwa na United.Nimeshinda kila kitu ndani na nje ya England.Miaka 6 niliyokaa pale haiwezi kufutika kwenye kumbukumbu zangu. Sasa nipo Madrid hivyo nategemea vyote nilivyoshinda nikiwa na United.

Utajisikiaje ikiwa Real Madrid watapangwa na Man United katika Champions League msimu ujao? Sitaki kucheza dhidi ya Manchester United, sitojisikia vizuri lakini huwezi kujua katika Champions League kila kitu kinawezekana lakini sipendi kucheza dhidi ya United.

Kina nani ni marafiki zako wakubwa ndani ya Manchester United? Bado nina marafiki walewale.Muda mwingine naongea Rooney, Vidic, Ferdinand, Nani, Evra, na Anderson.Ni vizuri kujua nini kinaendelea kule na watu wanapenda kujua kama nina furaha hapa na vitu vingine vinaendeleaje hapa.

Umehawi kumzungumzia Sir Alex Ferguson kama Baba yako katika soka.Mna mahusiano gani kwa sasa? Mr. Ferguson amenisaidia sana kukuza kipaji changu, nilikuwepo pale kwa miaka 6 na amenifundisha vitu vingi sana.Tumeshinda vitu vingi pamoja, namuheshimu sana, ni rafiki yangu na nampenda sana.

Matarajio yako yaliyobakia kwenye soka ni yapi? Matamanio yangu ni kushinda makombe mengi zaidi, binafsi na kwa timu yangu.Napenda kucheza soka, haya ni maisha yangu bila soka sijui nitafanya nini.Soka ni maisha yangu na nataka kushinda vitu iwezekanavyo.

Ungependa vitabu vya historia vikukumbuke vipi? Bado nina miaka 7 au 8 ya kucheza soka na kama bado nitakuwa na nguvu ningependa kucheza mpaka nifikishe miaka 40, hivyo nataka kuwa katika ukurasa wa kwanza wa historia kama ilivyo kwa Maradona na Pele.Nataka kuwa sehemu hiyo ingawa najua ni vigumu lakini nafikiri inawezekana kama nikiendelea kucheza hivi na kushinda mataji. ni vigumu lakini inawezekana, ipo kichwani na nitatimiza ndoto yangu.

No comments:

Post a Comment