Search This Blog

Saturday, June 4, 2011

NAIPENDA klabu ya Simba kiasili-MWANA FA











NAIPENDA klabu ya Simba kiasili, sitoweza kueleza ilikuaje nikaanza kuwa na mapenzi na timu hii”



Ndivyo anavyoanza kusema msanii Hamees Mwinjuma ‘MwanaFA’ kuhusiana na mapenzi yake kwa klabu ya Simba inayofahamika pia kama Wekundu wa Msimbazi.



Anasema anapendezwa na Simba kutokana uwezo mkubwa wa kucheza soka walionao wachezaji wengi wa timu hiyo, ambao baadhi yao ni marafiki zake.



Licha ya kuwa ni shabiki mkubwa wa Simba na msanii nyota wa Bongo Fleva, MwanaFA ni rafiki mkubwa wa wachezaji Juma Kaseja, Credo Mwaipopo na Athuman Idd ‘Chuji'. Pamoja na yote hayo, msanii huyu anavutiwa zaidi na uchezaji wa Kaseja.



“Kaseja, Credo na Chuji ni marafiki zangu wa ukweli na ndo maana mara kwa mara huwa nawatembelea nyumbani na hata wanapokua kambini,



“Nilianza kuingia uwanjani katika kila mechi ya Taifa Stars Kaseja aliporudishwa langoni, namuamini sana kipa huyu pindi anapowekwa katika nafasi yake,”

No comments:

Post a Comment