Search This Blog

Wednesday, June 1, 2011

MRWANDA NA ABDI KASSIM WAZUIWA KUJIUNGA NA STARS

Dan Mrwanda na Abdi Kassim ni miongoni wa wachezaji saba wanaocheza mpira wa kulipwa nje ya nchi walioitwa na kocha wa Taifa Stars, Jan Poulsen kwa ajili ya mechi dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati itakayofanyika Juni 5 mwaka huu jijini Bangui. Klabu yao ya Dong Tam Long ya Vietnam imekataa kuwaruhusu wachezaji hao kujiunga na Stars kwa madai kuwa iko kwenye hali ngumu katika ligi yao. Timu hiyo inashika nafasi ya mwisho kwenye ligi ya nchi hiyo inayoshirikisha timu 14, hivyo kudai kuwa wachezaji hao ni muhimu kwao kuwaokoa kutoka mkiani. TFF tumepinga hatua hiyo kwa vile ni kinyume na Kanuni ya Hadhi na Uhamisho wa Wachezaji (Regulations of Status and Players Transfer), hivyo tutawasilisha malalamiko yetu kwa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

No comments:

Post a Comment