Search This Blog

Thursday, June 2, 2011

TAFUTA TIMU YA KUICHEZEA MSIMU - FERGIE AMWAMBIA BROWN


Baada ya Owen Heagraves sasa Wes Brown amekuwa mchezaji wa pili kuangukiwa na panga la Sir Alex Ferguson ndani Old Trafford baada ya kuambiwa atafute timu ya kuichezea msimu ujao.

The Long serving defender mwenye umri wa miaka 31, amekuwa akiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara na hajaichezea United tangu alipoingizwa kama sub katika mechi na Bolton mwezi March mwaka huu.
Brown amepata upinzani mkubwa kutoka kwa Rafael, John Oshea na Fabio ambao wote wanacheza upande wa beki wa kulia.
Wes Brown ambaye alistaafu kuichezea timu yake ya taifa ya England in August 2010 na kuamua kuweka concentration yake katika kuitumikia klabu yake, alianza kuichezea Man United akiwa na miaka 18 mwaka 1998.

Msimu wake mzuri kipindi akiwa na United ni mwaka 2008 alipoichezea United katika michezo 50 na kufanikiwa kupata kombe la Champions League.

Timu ambazo zinaonyesha nia ya kutaka huduma za Brown ni pamoja na Everton na Sunderland.

No comments:

Post a Comment