Search This Blog

Friday, April 20, 2012

SABABU ZA BARCELONA KUSHUKA KIWANGO

Kila nabii ana nyakati yake , nyakati ambazo huanza taratibu na baada ya muda uwe mrefu au mfupi nyakati hizi hufikia mwisho . Vivyo hivyo kila falme hakika ina zama zake m zama ambazo zina mwanzo na mwisho . Kwenye soka kumekuwa na falme mbalimbali ambazo huwekwa na timu tofauti kwa nyakati tofauti.

 Wakati soka la ushindani kwa maana ya soka la kimataifa lilipoanza mwishoni mwa miaka ya 20 timu ya taifa ya Uruguay ndio ilikuwa baba wa soka ulimwenguni, Uruguay mpaka kufikia mwaka ambao kombe la dunia lilichezwa kwa mara ya kwanza likuwa imeshatwaa ubingwa wa michuano ya olimpiki mara mbili na waliendeleza  ubabe wao mwaka wa kombe la dunia ambapo walitwaa ubingwa wa kwanza wa kombe la dunia.

 Baada ya hapo Italia waliingia kwa muda mfupi ambapo walitwaa kombe la dunia mara mbili katika miaka ya 1934 na 38 . Kwenye miaka ya 50 Uruguay walirudi kwa muda kabla ya kuwapisha wababe wapya Brazil ambao walitawala kipindi cha kati ya miaka 1958 mpaka 1970.

 Katika miaka yote hiyo timu zimekuja na kundoka na kuja na kuondoka tena lakini hakuna hata moja ambayo ufalme wake ulidumu milele.
Kwa upande wa vilabu Real Madrid waliatawala sana miaka ya kuanzia 1955 mpaka 70 kabla ya timu nyingine kama Ajax , Liverpool, Bayern Munich na Ac Milan mpaka kufikia kati ya muongo wa 1990 .

Katika miaka ya 2000 hakuna klabu ambayo imetawala mchezo wa soka barani ulaya kama Fc Barcelona . Hata kabla ya uji wa Pep Guardiola Barca walikuwa wanatisha wakiwa na safu ya hatari ya kiungo na ushambuliaji ambayo ilikuwa na watu kama Ronaldinho Gaucho ,Samuel Etoo ,Thierry Henry, Deco , Henrik Larson, na wengineo wengi . Kizazi hicho kilipita kikaja kizazi cha kina Lionel Messi , Sergio Busquets , Pedro Rodriguez, Gerard Pique ambao waliungana na wakongwe waliokuwepo tangu wakati wa Rijkaard kina Carles Puyol , Xavi Hernandez na Andres Iniesta pamoja na baadhi ya wachezaji walionunuliwa kama Eric Abidal , Seydou Keita na wengine .
Katika vipindi vyote hivi Barcelona imetawala bila kupingwa huku ikitwaa ubingwa wa Ulaya mara tatu tangu mwaka 2006 na mataji manne ya ligi ya nyumbani.

 Hata hivyo alipokuja Pep Guardiola ndio Barcelona inaonekana kushika kasi kuliko hata hapo awali. Chini ya Pep Barca imetwaa mataji 13 kati ya 16 ambayo imeshiriki huku Lionel Messi akiibuka kama mchezaji bora pasipo kipingamizi chochote .
Hata hivyo utawala huu wa Barcelona hatimaye unaonyesha dalili mbaya za kuanza kufifia taratibu.

 Hii si kusema kuwa Barcelona wameshuka kufikia kiwango kibaya kama ilivyokuwa kwa timu kama Ac na Inter Milan au hata Man United ambayo msimu huu umekuwa mbaya sana kwake hasa kwenye michuano ya ulaya.

 Pamoja na hayo Barcelona msimu huu hawajarejea kwenye kiwango cha kutwaa mataji yote inayoshiriki kama msimu uliopita na hata misimu miwili mitatu nyuma.
Kuna sababu mbalimbali ambazo zinaonekana kutishia ufalme wa Barcelona .
Ukiangalia Barcelona ya sasa bado ina watu muhimu kama Xavi, Iniesta, Messi na Puyol.

 Hata hivyo tofauti iliyoko sasa na Barcelona ile ya mwaka 2009 ambayo iliilaza Man United maba mawili bila pale Rome utagundua jambo moja kubwa . Barcelona ya sasa inamtegemea sana Lionel Messi tofauti na miaka mitatu iliyopita . Inawezekana kuwa Messi kwa sasa amekuwa kiuchezaji tofauti na hapo awali lakini ukweli unabaki kuwa Barca inamtegemea sana kijana huyu toka Rosario Argentina.

Hadi kufikia mwisho wa msimu wa mwaka 2008-2009 Fc Barcelona ilitwaa ubingwa wa La Liga huku ikiwa na uwiano wa ufungaji wa mabao mzuri ambao ulikuwa umesambaa kwa wachezaji watatu. 

Samuel Etoo alikuwa na mabao 31, Leo Messi alikuwa na mabao 23 na Thierry Henry alikuwa na mabao 19 , hii ilitengeneza jumla ya mabao 74. Wingi wa mabao ya jumla sio hoja kuu ila jinsi mabao haya yalivyosambaa kwa wachezaji wengi na sio mmoja.

 Ukiangalia takwimu za ufungaji zinavyoonyesha msimu huu utaona Leo Messi ana mabao 41, Xavi Hernandez na Alexis Sanchez wakiwa na mabao 10 kila mmoja . Tofauti ya mabao ya jumla kwa mara nyingine sio hoja kwani ukiangalia jumla ya mabao ni 70 huku tofauti ikiwa ndogo tu ya mabao manne.

 Hata hivyo tofauti kubwa ambayo inaogopesha hapa ni ukweli kwamba Messi peke yake ana mabao 41 na anayefuatia ana mabao 10. Ishara inayopatikana hapa ni kwamba Barcelona si lolote s chochote bila Messi. Rudi nyuma kwenye mwaka huo huo wa 2009 halafu angalia hali ilivyokuwa kwa mahasimu wa Barca Real. Takwimu zao zilinyesha kuwa mfungaji bora alikuwa Gonzalo Higuein akiwa na mabao 22 akifuatiwa na Raul Gonzalez akiwa na mabao 18. Baada ya hapo angalia takwimu za Real mwaka huu Cristiano Ronaldo ana mabao 41 , Gonzalo Higuein ana 22 na Karim Benzema ana 18 . Kwa mara nyingine tena jumla ya mabao si issue kubwa ila mgawanyo wa mabao kwa maana ya kwamba Real hawana tatizo lililoko Barcelona la kuwa tegemezi sana kwa Messi.

Hili si tatizo ambalo linaikuba Barca kwenye La Liga peke yake bali hata kwenye Ligi ya mabingwa . Msimu ambao Barca ilitwaa ubingwa kwa kuifunga Man United mabao mawili kule Rome Messi alikuwa na na mabao 9, Henry mabao matano na Etoo Manne. Msimu huu Messi ana mabao 14 huku anayefuatia akiwa pedro mwenye mabao manne . Kwa upande wa Real kwa mara nyingine mabao yamegawanyika kwa wachezaji wengi , Ronaldo ana nane , Benzema ana saba , Jose Callejon ana mabao matano , Kaka na Higuein wana matatu kila mmoja. Picha unayoipata hapa ni kwamba Bila Messi Barcelona sio Barcelona lakini kwa Madrid bila Ronaldo Benzema atafunga na Higuein atafunga.

 Haimaanishi kuwa Barca hawana watu wa kufunga ila mabao yanayofungwa na wachezaji wengine ni machache sana kiasi cha kuifanya timu kuwa tofauti.
Ukweli wa hoja hii unapatikana kwenye mchezo wa jumatano kati ya Chelsea  na Barcelona . Kila ambapo Lionel Messi aligusa mpira angezungukwa na wachezaji wawili watatu, matokeo yake yalikuwa Barcelona kufungwa.

 Japo waligongesha sana miamba lakini takwimu zinaonyesha kuwa mabao yanayofungwa na wengine hayatoshi na juu ya yote Messi ndio chief goalscorer jambo ambalo hata wachezaji wengine wa Barcelona wanaonekana wamelizoea.

Sababu ya pili kubwa ya ufalme wa Barca kufikia ukomo muda si mrefu ni ya kipuuzi sana lakini ina kila chembe chembe ya ukweli ndani yake . Mafanikio makubwa ambayo Barca imeyapata ndio sababu kuu ya waokushindwa kupata mafanikio mengine zaidi . Katika hali ya kawaida ni rahisi sana kupanda ngazi za mafanikio , lakini ni kazi ngumu sana kuendelea kubaki kwenye kilele cha mafanikio hasa pale ambapo mafanikio haya yamekuwa yakija kwa staili kama ambayo Barca ya Guardiola imepata mafanikio yake.


Mataji 13 kwenye mashindano 16 ambayo Barca imeshiriki kwa kipindi cha miaka yake mitatu ni mafanikio makubwa  sana kwa kipindi kidogo na kiukweli ni vigumu sana kwa wachezaji wa Barcelona kwa ujumla kupata sababu ya kutafuta nguvu ya ziada ya kuendelea kufanya vizuri baada ya mafanikio ya muda mfupi, hili ni jambo ambalo hata Pep Guardiola mwenyewe amekiri .

Wakati Barcelona inatwaa ubingwa wa Champions League mwaka 2009 Kazi kubwa sana ilikuwa imefanywa na Samuel Etoo japo messi alimaliza kama mfungaji bora wa michuano hiyo lakini Etoo ndiye alikuwa mfungaji bora wa michuano yote hivyo Lionel Messi ambaye ndio kwanza alikuwa anachipukia alikuwa na sababu ya kufanya vyema zaidi baada ya hapo kutokana na kuhisi kuwa mafanikio ambayo Barca iliyapata hayakuwa na mhuri wake kama mchezaji mwenye mchango mkubwa na ndio maana baada ya hapo Messi alifanya kazi kubwa ya kufika hapa alipo.

 Tofauti iliyopo sasa ni kwamba wachezaji kama Alexis Sanchez na Cesc Fabregas ambao wako kwenye msimu wao wa kwanza wana wakati mgumu sana kufanya yale aliyofanya Messi na hapo ndio unapokuja ukweli wa hoja hii ya kutafuta mafanikio ya kwako kama mchezaji badala ya yale ya timu.

Na zaidi ya hayo njia ya mafanikio ni kama mlima, wakati wewe unapanda unapishana na watu wanaoshuka na wakati utafika ambapo na ewe utashuka huku ukipishana na watu wanaopanda na kwa jinsi Barcelona walivyopata mafanikio yake kuna timu nyingine zitajipanga na kuwa bora kwa nyakati todauti na hii itamaanisha kutoa ushindani mkubwa sana kwa Barcelona jambo ambalo ukiunganisha na sababu nyingine zilizotajwa hakika zitachangia kushuka kwa ufalme wa Barcelona.

 Mfano wa hili ni jinsi Real Madrid walivyowapa upinzani mkubwa Barcelona kwenye La liga na hata kwenye ligi ya mabingwa . Tegemea hili kwenye michuano ya ulaya ambako timu kama Bayern Munich, Manchester United,Ac Milan zote zitawatazama Barcelona na kujipanga.

Mwisho wa siku haya yote yanaweza yakawa imani tu au propaganda dhidi ya Barcelona ambayo kiukweli inabakia kuwa timu bora ya kizazi hiki lakini ubora huu utafikia ukomo wake. Na ukomo huu umeanza kuonyesha ishara zake .

12 comments:

  1. Eh!Barca wameshuka kiwango tena? Ni baada ya kufungwa na Chelsi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Performance yao sio ile tuliyoizoea, wamepungua uwezo kiukweli

      Delete
  2. Hawajashuka... wanaelekea kufika mwisho wa utawala wao!! we check game tatu zilizopita walizocheza na madrid!! yani game inakuwa 50/50 wakat few years back walikuwa wanawanyanyasa wanavyotaka!! Mwisho wao unakaribia kwanza timu pinzani zinajipanga kuogopa humiliation plus Ivumayo haidumu believe or not

    ReplyDelete
  3. Ama hakika kazi wanayo. Na ndo mana kila siku ina jina.

    ReplyDelete
  4. Kaka asante kwa uchambuz wako...
    Ni uchambuz mzuri na wenye uweled..
    ILA MKUU TUNAOMBA UTUMIE BLACK-KWENYE FONT COLOUR.
    Nimesoma habari yote ila macho yanaumia sana kusomea kwenye red na ukitazama ni kitu interesting amabcho mtu wataka soma hoja nzima

    ReplyDelete
  5. Dah shaffii sasa kufungwa na madri na chellsea ndo wameshuka kiwango dah tumeishiwa wachambuzi wa soka inaonesha ni jinsi gani una chuki na barcelona

    ReplyDelete
  6. "Diminishing maginal utility" it means wamekunywa maji mengi sana so kiu hakuna tena. Lazima wa re_new timu upya

    ReplyDelete
  7. ndo soka kungkw hakuna radha km m2 anashnda yy 2 kila cku...

    ReplyDelete
  8. Kwa juu walipofika Barca hata wakishuka kufika chini sio leo...!!

    ReplyDelete
  9. Barcelona hawajashuka kiwango aslani. Mi game nyingi za Barca huwa naziwatch, bado wapo kwenye peak nzuri na hawafananishiki na club yoyote duniani! Jana Tello amewacost kweli yaani. Amepata nafasi nzuri ameshindwa kuzitumia. SHAFFIH, Barcelona ni wazuri!

    ReplyDelete
  10. mhh nimekusoma vizuri na nimekuelewaa sana lakini hayo ni mawazo yako kama binadamu wengine kila mtu anauwezo wa kutoa mawazo yake but for me i dont think so still barc bado wapo mapa elfu mbili na kumi na tano au na sita kama huamini just stay and watch and u will realize that kipindi akiondoka rijkard barc ili shake sana tu na watu wakaongea kama ww hivyo ulivyo sema kikowapi so usianze kuongea mapema kwa barc kufungwa mechi nne kwenye msimu moja subiri msimu ujao ukiisha akiwa kafanya vibaya toa maoni yako kwani barc ndiyo timu ambayo uliambiwa haitaka ifungwe acheni habari zenu

    ReplyDelete
  11. Hilo lipo wazi kuwa barca wanaporomoka na dawa yao nadhani imepatikana kuwa ni kujiamini,kupaki basi na kujiangusha kama wao then mambo yanaenda,....kaka Shaffih vp kuhusu man utd?

    ReplyDelete