Search This Blog

Friday, July 29, 2011

BREAKING NEWZ: BANKA AASTAFU SOKA


Kiungo mkongwe wa Simba, Mohamed Banka aliyetolewa kwa mkopo Villa Squad amesema ameamua kuipa kisogo soka na kujikita kwenye biashara.
Uongozi wa Simba ulikutana na Banka juzi ili asaini mkataba mpya na waanze upya, lakini kiungo huyo aligoma kwa madai kuwa hawezi kucheza tena klabu iliyojaa majungu na maneno ya kila siku yasiyoisha.
Awali Simba ilitangaza kumpeleka kwa mkopo kiungo huyo kwenye timu ya Villa Squad kwa ajili ya kuimarisha kipaji chake, lakini mchezaji huyo amegoma na kwa sasa amejikita kwenye shughuli zake binafsi.

"Kiwango changu hakijaisha mpaka waniambie eti nikaimarishe kiwango, mimi sio wa kiivyo, wao walidhani wananikomoa kumbe wanajikomoa wenyewe mimi sasa hivi nafanya biashara zangu, tena imekuwa vizuri kwa kuwa napata muda mzuri wa kuzisimamia na kuziimarisha,"alisema Banka.

"Juzi baada ya kupeleka barua TFF waliniita na kutaka tuyamalize tuanze upya kwa kusaini mkataba mwingine, lakini siwezi, sina tena moyo wa kuichezea Simba, wamekuwa wakinituhumu mara kibao kuwa mimi ni Yanga, kila kitu kibaya wananiambia mimi, ni bora nisicheze mpira lakini niwe na amani kuliko nikae mahali sina amani, acha nifanye biashara zangu."alisisitiza Banka.

Alisema kilichomsababisha mpaka akaamua kuushtaki uongozi wa Simba TFF ni kitendo chao cha kuchelewesha kumtangaza kumuacha ili atafute timu nyingine na badala yake wamemuacha dakika za mwisho tayari usajili umeshapita hivyo anachotaka Simba wamlipe fidia na pia wavunje mkataba wake ili aweze kuangalia maslahi mengine.

source:www.mwananchi.co.tz

2 comments:

  1. Kwa maoni yangu na jinsi nilivyokuwa namfuatilia Banka, ni kweli kiwango kimeshuka hasa msimu huu wa 2010/2011, si timu ya taifa wala simba, mi nahisi majeruhi au majeraha ambayo yanamuandama, mi nafikiri apunzike ili apone kwanza, tumeona Mwakingwe aliamua kupunzika kwa nusu msimu na sasa karudi kwa kasi kubwa, au je kapigwa misumari au hata yeye kuwapiga wenzake.Namshauri ajiulize ni wapi alipojikwaa sio alipoangukia na kubaki kutoa maneno ya kashfa kwani simba walimtoa sana tu baada ya kuachwa na yanga.U heard?

    ReplyDelete
  2. Banka afanye maamuzi ya busara ili naye asikosee kama anavyodai Simba wamekosea. Nani alijua leo akina Ngasa na Nizar wangefika walipo bila kuwa Simba na Yanga? Siafiki sana uamuzi wa kuachana na soka kwa sasa, hakuna ajuaye ni lini naye angeweza kuwa wapi!

    ReplyDelete