Search This Blog

Tuesday, July 26, 2011

DAVID GILL:UNITED TUTASAJILI MCHEZAJI MMOJA TU WA DARAJA LA JUU


Afisa mkuu wa klabu ya Manchester United David Gill amethibitisha kuwa klabu yake inajiandaa kusajili mchezaji mmoja mwenye hadhi ya juu katika kipindi hiki cha usajili.

Red Devils tayari wameshajili wachezaji watatu katika kipindi hiki cha usajili, Golikipa David De Gea akimrithi Van Der Sar, huku Ashley Young na Phil Jones wakiongezwa kuimarisha kikosi kwenye ulinzi na ushambuliaji.

Sir Alex Ferguson juzi aliweka wazi kuwa hakuna uhakika wa kuwepo kwa usajili mpya kabla ya mchezo wa ngao ya hisani at Wembley mwezi ujao tarehe 14, na sasa Gill amekiri kuwa hakuna usajili utakaofanyika katika siku za karibuni, ingawa CEO huyo amewahakikishia mashabiki na wapenzi wa United kuwa watafanya usajili wa mchezaji mmoja kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili August 31.

“Van Der Sar alisema mapema kuwa msimu uliopita ndio ulikuwa wa mwisho, hivyo tulijipanga kusajili golikipa, na nafasi nyingine zilipotokea tulizijaza vizuri,” aliiambia MUTV.

“Mpaka sasa tumesajili wachezaji watatu, nab ado tunajiandaa kusajili mwingine mmoja.

“Hakuna kinachofanyika kwa sasa, lakini tutaona nini kitatokea tutakaporudi nyumbani.Bado kuna siku zaidi ya 31 za dirisha la usajili, kwahiyo chochote kinaweza kutokea.Lakini kwa sasa sishughulikii na uhamisho wowote.”

Gill pia amethibitisha kuwa Ferguson anajiandaa kuimarisha sehemu Fulani ya kikosi, huku nafasi ya kiungo mshambuliaji ikitajwa sana kufuatia kustaafu kwa Paul Scholes.

Samir Nasri na kiungo mchezeshaji wa Tottenham Luka Modric wote wamekuwa wakihusishwa na United, huku speculation zikiendelea kuhusu kiungo wa kidachi wa Inter Milan Wesley Sneijder.

Wakati Gill akikataa kutaja mchezaji wanayemuwania, lakini United CEO amekiri kuwa ni mchezaji mwenye daraja la juu pekee ndio atakuwa anahitajika ndani kikosi cha Red Devils.

“Tumekuwa tukiwafuatilia wachezaji wawili au 3 wa nafasi moja, lakini mpaka sasa hakijafanyika kitu juu ya usajili wa mchezaji huyo.Suala muhimu ni kuwa Alex ameweka wazi kwamba tunahitaji mtu ambaye atakuja kusaidia kuongeza ubora wa kikosi.

“Tuna kikosi kizuri na kikubwa na ili uweze kupata nafasi ya kuingia ndani ya kikosi hicho inabidi uwe mchezaji wa daraja la juu.” Alimaliza David Gill.

No comments:

Post a Comment