Search This Blog

Thursday, July 28, 2011

Ngassa arejea nyumbani,ATAJIUNGA RASMI NA SOUNDERS FEBRUARY MWAKANI KWA AJILI YA MAANDALIZI YA MSIMU UJAO !




Mrisho Ngassa alikuja Seattle Sounders Fc kufanya majaribio kama sehemu ya juhudi za klabu ya Seattle Sounders kuongeza wigo wake kwenye masuala ya uskauti kwenye eneo la Afrika Mashariki.
Kwenye dakika ya 76 ya mchezo wa kirafiki baina ya Seattle Sounders na klabu bingwa ya England Manchester United wachezaji watatu waliingia kwa upande wa Seattle Sounders.
Miguel Montana mchezaji mwenye umri wa miaka 20 toka Colombia ni mmojawapo wa waliopata nafasi ya kuonyesha uwezo wao dhidi ya mojawapo kati ya vilabu vikubwa duniani Manchester United.
Mwingine alikuwa O’Brian White ambaye huu ulikuwa mchezo wake wa kwanza tangu alipotolewa uvimbe wa damu kwenye mguu wake mwezi aprili .
Kivutio kilikuwa mchezaji wa tatu kwenye orodha hii ya wachezaji walioingia . Mrisho Ngassa aliingia akicheza kwenye eneo la kiungo wa upande wa kulia. Kuingia kwake kulikuwa kama hakuna maana ukizingatia kuwa tayari timu aliyopaswa kuchezea siku hiyo ilikuwa tayari imesharudi wavuni mara sita .
Ngassa aliingia kwa upande wa Sounders kama mchezaji anayefanya majaribio toka klabu ya ligi kuu nchini Tanzania Azam Fc .
Majaribio haya ya Ngassa yamejengwa kwa muda wa mwaka mmoja mzima. Seattle Sounders wamekuwa wakitengeneza mahusiano na nchi ya Tanzania tangu walipokuja mara ya kwanza msimu uliopita . Kocha msaidizi wa Seattle Sounders na mkuu wa maskauti au wasaka vipaji wa Seattle Kurt Schmid alifunga safari hadi nchini Tanzania mwaka jana kutazama mchezo na mazoezi ya timu ya Taifa ya Tanzania . Akisaidiwa na kupewa ushauri na kocha wa timu ya taifa Jan Poulsen , Schmid alimchagua Ngassa kama mchezaji aliyemvutia na atakayempa nafasi ya kufanya majaribio kwenye timu yake ya Seattle Sounders .
“Unapokwenda sehemu kama Tanzania na kumuona mtu ambaye amewazidi wenzie kwa mambo karibu yote ni lazima uulize kwanini? Alisema Schmid.
Jibu la swali la Schmid, kwanini Ngassa lilikuwa kwenye kasi na kipaji kilichopo kwenye miguu yake .
Akiwa na kimo kidogo cha futi 5 , Ngassa anatumia vyema kasi aliyo nayo kuwapita mabeki akiwapiga chenga za akili huku akiwatengenezea wenzie nafasi za kufunga . Hata kwenye mechi dhidi ya Man United kwa dakika chache alizopata za kuonyesha uwezo wake aliweza kupiga shuti moja , ambapo alikosa nafasi iliyookolewa na Rio Ferdinand .
“Ngassa ni mtu mwenye umbo dogo, ila tuna uzoefu wa kuwa na wachezaji wenye vimo vidogo ambao wanafanya vizuri na timu zao na hata kwetu pia na wanacheza vizuri tu. Ana kasi ya ajabu, nadhani kasi yake kwenye mbio fupi ni hatari sana , anasema Schmid,ana uwezo mkubwa sana kiufundi , anaweza kuwapiga chenga mabeki na kupiga mashuti pia. Ana uwezo wa kuusoma mchezo vizuri ila anahitaji kuwa na juhudi kwenye ukabaji kidogo ili akamilike kiuchezaji.
Huku kukiwa na ishara zote juu ya matunda ambayo yanaweza kuchumwa na Seattle Sounders kama matunda ya uhusiano wake na Tanzania , faida haitakuja kwa Seattle Sounders peke yake . Kwa mujibu wa Mmiliki wa Klabu ya African Lyon Rahim Zamunda Kangezi ambaye alikuwa sambamba na Ngassa kwenye safari yake nchini Marekani , nafasi kwa Seattle na Vilabu vingine vya MLS zitaongeza sifa na wigo wa soka la Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki kama ilivyofanya nchi ya Ufaransa kwa nchi za Afrika Magharibi.
“Vipaji ni vile vile kama vya Afrika Magharibi ila tofauti ni kwamba Afrika Magharibi wana mahusiano na nchi ya Ufaransa . Sounders inawapa nafasi kama hii wachezaji wa Afrika Mashariki kwa kutumia mahusiano na nchi za Afrika Mashariki , alisema Zamunda . “Unapozungumzia soka barani Afrika ni ndoto ya kila mchezaji . Kuwaona wachezaji hawa wakija Marekani kucheza soka ni faraja kubwa sana kwa soka letu.
Seattle Sounders wanakubali kuwa nguvu iliyoko kwenye uhusiano wa vilabu vya Marekani na wawakilishi toka Tanzania itasaidia kuleta mambo mazuri zaidi na yanaweza kuleta vipaji zaidi toka mahali ambako MLS bado haijapagusa .
“Tanzania ni mahali ambako hapajaguswa . Kuna watu wanaotoka sehemu hii wanaocheza Ubelgiji na Norway ambao wamezunguka sehemu mbalimbali ulimwenguni alisema Schmid,. Nadhani ni sehemu ambayo kuna vipaji vingi vya asili na hakika kuna watu wanaojua kucheza huko , kunahitaji maendeleo tu zaidi na kwa uhusiano huu kuna mengi mazuri yanakuja na tutawaendeleza wachezaji hawa.
Ngassa anatarajiwa kurudi Tanzania baadae na atarejea mnamo mwezi February mwakani kujiunga na Seattle Sounders kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa mwaka 2012.


SOURCE: www.soundersfc.com

No comments:

Post a Comment