Beki wa zamani wa vilabu vya Yanga,Pan African na Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Omary ‘Mwamba ‘ Kapera ameiomba Serikali kuwaangalia kwa ukaribu wanamichezo wa zamani ambao kwasasa wanasumbuliwa na maradhi mbali mbali walioliletea sifa Taifa letu kupitia michezo hasa mchezo wa soka. Kapera ambaye kwasasa anasumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi pia amemuomba Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete na Serikali yake kutafuta namna ya kuwasaidia wanamichezo wa zamani.
Huyu ndo Mwamba Kapera enzi zake....
Hapa namnukuu Kapera ‘’Nilipata Stroke ya mwili nikaanguka lakini bahati nzuri nimejitibu kwa kushirikiana na watoto wangu walau nimepata nafuu,lakini bado sijapona kabisa na hilo ndilo tatizo kubwa linalonikabili kwasasa,na katika kipindi chote cha kuugua nimekuwa nikipata msaada mkubwa kutoka kwa watoto lakini sipati msaada kutoka Serikani,silazimishi lakini kati ya watu wanaoangaliwa kwa ukaribu na serikali basi nasisi wachezaji wa zamani tuangaliwe’’. Omary Kapera alikuwa Sentahafu maarufu wa vilabu vya Yanga,Pan African na timu ya Taifa alikuwa maarufu kwa jina la ‘Mwamba’ kutokana na umahili wake wa kuwazuia washambuliaji wakali kama Willy Mwaijibe,Adam Sabu na Khalid Abeid. Mwamba Kapera aliendelea kunena yafuatayo,’‘Raisi Kikwete juzi juzi amewatunuku wasanii kina Muhidini Gurumo na Bi Kidude tunashukuru amefanya vizuri lakini arudi na kwa wachezaji na sisi tufarijike kwa namna moja ama nyingine,ni hilo tu’’
Hivi ndivyo Mwamba Kapera alivyo hivi sasa.....hapa nilimtembelea nyumbani kwake.
Kama ningepata nafasi ya kukutana ana kwa ana na Raisi Kikwete ningemwambia atuangalie wachezaji wazamani tunaoumwa na hata wale wazima,atuangalie kwa ukaribu kwani hali zetu siyo nzuri,kutuangalia haina maana kwamba Raisi Kikwete ndiye atuangalie, hapan yeye atoe amri,akitoa amri wapo watu watakaofanya iyo kazi kwa niaba yake’ Kapera pia amesema hana sababu ya kukumbuka mema aliyofanya akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania, ‘‘
'' Nimeichezea timu ya Taifa kwa muda mrefu lakini haaa! siikumbuki kwasababu na wao hawanikumbuki namimi siikumbuki,Yanga ni kama Nyumbani nimeichezea Yanga kwa kipindi cha miaka kumi,nimelelewa na YANGA,Yanga imenifanya nimetembee duniani kote,sikupata kitu lakini nilijitangaza na umaarufu wangu wote niliupata kwasababu ya Yanga kwaiyo nina haki ya Kuisemea ‘’
Search This Blog
Monday, January 7, 2013
AFCON 2012: YAYA TOURE AUGUA GHAFLA ABU DHABI - ALAZWA
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa fainali za mataifa huru ya Afrika huko nchini Afrika ya Kusini, mchezaji bora wa bara la Afrika Yaya Toure ameugua ghafla kifua na homa kali na sasa amelazwa katika hospitali moja huko Abu Dhabi walipoweka kambi na timu yake ya taifa ya Ivory Coast.
Kikosi cha Ivory Coast kiliwasili UAE siku ya jumamosi wakitokea Paris, wakati timu ilipokutana na maofisa wengine kabla ya kwenda Uarabuni.
Toure hakuwepo kwenye mazoezi ya kawaida ya timu hiyo siku ya jumapili, wakati maofisa wa afya wa timu hiyo wakijaribu kufanya kazi ya ziada kuweza kuirejesha hali ya mchezaji kwenye usawa huku wakishindwa kusema ni lini atarudi mazoezini.
Nahodha wa timu hiyo Didier Drogba pia hakuweza kufanya mazoezi jana kwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya kichwa.
Ivory Coast watacheza mechi ya kirafiki na Egypt January 14 kabla ya kusafiri kwenda South Africa siku mbili baadae kwa ajili ya AFCON 2012.
Kikosi cha Ivory Coast kiliwasili UAE siku ya jumamosi wakitokea Paris, wakati timu ilipokutana na maofisa wengine kabla ya kwenda Uarabuni.
Toure hakuwepo kwenye mazoezi ya kawaida ya timu hiyo siku ya jumapili, wakati maofisa wa afya wa timu hiyo wakijaribu kufanya kazi ya ziada kuweza kuirejesha hali ya mchezaji kwenye usawa huku wakishindwa kusema ni lini atarudi mazoezini.
Nahodha wa timu hiyo Didier Drogba pia hakuweza kufanya mazoezi jana kwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya kichwa.
Ivory Coast watacheza mechi ya kirafiki na Egypt January 14 kabla ya kusafiri kwenda South Africa siku mbili baadae kwa ajili ya AFCON 2012.
ITSSSSSS MESSI AGAIN - AWAFUNIKA RONALDO NA INIESTA NA KUVUNJA REKODI YA KUCHUKUA BALLON D'OR KWA MARA 4 MFULULIZO
![]() |
| Lionel Messi - Kiboko asiyeshindika |
![]() |
| Wapinzani |
![]() |
| Kocha Bora wa Mwaka Vicente Del Bosque |
![]() |
| Timu bora ya Mwaka |
Ronaldo na Messi wakivunja rekodi ya kuwemo kwenye kikosi hicho kwa mara 6 mfululizo. Casillas ameingia mara 5.
Wachezaji wanaounda timu hiyo ni -
Goalkeeper: Iker Casillas
Defenders: Dani Alves, Gerard Pique, Sergio Ramos, Marcelo
Midfielders: Xabi Alonso, Xavi Hernandez, Andres Iniesta
Forwards: Lionel Messi, Radomel Falcao, Cristiano Ronaldo
KALI YA LEO: IKER CASILLAS ALIPOKATAA KITAMBAA CHA UNAHODHA KUTOKA KWA CRISTIANO RONALDO
Kama alivyofanya katika mchezo wa mwisho kabla ya mwaka kuisha, Jose Mourinho aliamua kumpiga benchi tena golikipa Iker Casillas katika mchezo wa kufungua mwaka dhidi ya Real Sociedad. Wakati huu, kwa bahati mbaya mambo hayakwenda kama Mourinho alivyotaka.
Kipa aliyeanza Antonio Adan alionyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya sita, na kumlazimu Mourinho kumuingiza Casillas kwenye mchezo huo. Pmaoja na adhabu ya penati waliyopewa kutoka na faulo aliyofanya Adan, Sociedad walienda na kufunga mara mbili katika kipindi cha kwanza wakichuana vikali na Madrid.
Lakini baada ya penati kupigwa kitu kisicho cha kawaida kikatokea. Cristiano Ronaldo akiwa amevaa kitambaa cha unahodha kwa mara ya kwanza kwenye mechi rasmi ya mashindano, alikivua kitambaa hicho na kwenda kumpeleka Casillas katika dakika ya 12 ya mchezo. Casillas akakataa na kumsukuma Ronaldo, hivyo Ronaldo akakivaa tena kitambaa na kuendelea na mchezo ulioisha kwa 4-3 huku Ronnie akifunga mabao mawili.
Kipa aliyeanza Antonio Adan alionyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya sita, na kumlazimu Mourinho kumuingiza Casillas kwenye mchezo huo. Pmaoja na adhabu ya penati waliyopewa kutoka na faulo aliyofanya Adan, Sociedad walienda na kufunga mara mbili katika kipindi cha kwanza wakichuana vikali na Madrid.
Lakini baada ya penati kupigwa kitu kisicho cha kawaida kikatokea. Cristiano Ronaldo akiwa amevaa kitambaa cha unahodha kwa mara ya kwanza kwenye mechi rasmi ya mashindano, alikivua kitambaa hicho na kwenda kumpeleka Casillas katika dakika ya 12 ya mchezo. Casillas akakataa na kumsukuma Ronaldo, hivyo Ronaldo akakivaa tena kitambaa na kuendelea na mchezo ulioisha kwa 4-3 huku Ronnie akifunga mabao mawili.
YANGA DIMBANI DHIDI YA DENIZLISPOR KESHO

Timu
ya Young Africans Sports Club kesho itashuka dimbani kucheza na timu
ya Denizlispor FC ya ligi daraja la kwanza nchini Uturuki katika mchezo
wa kirafiki utakaofanyika katika uwanja wa Selen Football -Kalimya
Complex pembeni kidogo ya mji wa Antlaya.
Young Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo
jijini Antalya itatumia mchezo huo kama fursa ya kujipima nguvu na timu
hiyo la Denizlispor FC ambayo imeshuka kutoka ligi kuu ya Uturuki mwaka
jana na hivi sasa inapamabana kurudi tena katika Ligi Kuu ya Uturuki.
Kocha
Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kupata
nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Denizlispor FC ambayo ina
wachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo anaamini utakua ni mchezo safi
na kuwavutia.
Baada ya kuwa na
wiki moja ya mazoezi na mechi moja ya kirafiki dhidi ya Armini Bielefeld
ya ujerumani mwishoni mwa wiki itakua ni fursa nyingine nzuri ya
kucheza mchezo wa kirafiki na timu nyingine, hii itanisadia kuona
maendeleo ya kikosi changu kutokana na mazoezi ambayo tumekuwa
tukiyafanya tangu tulipofika alisema 'Brandts'
Denizlispor
FC ni miongoni mwa timu zaidi ya 200 kutoka shemu tofauti duniani
ambazo zimeweka kambi katika mji wa Antlaya kwa ajili ya maandilizi ya
mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la kwanza nchini Uturuki.
Mchezaji
wa zamani wa Leicester City ya Uingereza, Dundee United ya Scotland na
Ivernes ya Uholanzi, mtanzania mzaliwa wa Uingereza Eric Odhiambo ni
miongoni mwa washambuliaji wa kutegemewa wa timu ya Denizlispor FC.
Young
Africans imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari
kabisa kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa kesho katika uwanja wa Selen
Football - Kalimya complex pemebeni kidogo ya mji wa Antalya.
Kikosi
cha wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na
hakuna maheruhi hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia
mchezaji yoyote katika mchezo huo.
Athumani Idd
'Chuji' na Hamis Kiiza waliokuwa wakijisikia vibaya kabla ya mchezo wa
juzi dhidi ya Amrnini Bielefeld wanaendelea vizrui kabisa kwani
wanaendelea na mazoezi pamoja na wachezaji wengine waliopo na timu mjini
Antalya.
Kuhusu hali ya hewa leo haijaonekana
kuwa tatizo kwa wachezaji kwani wanaonekana kuimudu na mda mwingi kwa
sasa kumekua na jua linalowaka kuanzia asubuhu wakati wa mazoezi mpaka
mida ya jioni, kwa leo hali ya hewa ni nyuzi joto 17 - 21, hivyo hali ya
hewa ni nzuri kabisa na jua linawaka mda wote.
SOURCE:youngafrican.co.tz
JUMA OMARY- ' NILIUZA SUPRA ZANGU ILI NIPATE NAULI YA KUJA DAR KUCHEZA SOKA'

Katika sehemu ya kwanza ya story hii ya kijana wa kitanzania kutoka mkoani Katavi Juma Karim Omary akielezea namna alivyokuwa akitafuta njia ya kuweza kufanikiwa kisoka akiwa mkoani kwao baada ya kufeli kimasomo, hivyo akaamua kudhamiria kujituma ili mpira uweze kuwa ajira yake. Sehemu ya pili ya stori tutaona namna kijana huyo alivyoweza kusafiri kutoka Katavi mpaka kufika Dar es Salaam.
Juma anasema sio kwamba hakuwa anapenda shule kama apendavyo soka, bali kulitokea matatizo wakati akifanya mitihani yake ya kumaliza elimu ya sekondari hivyo akajikuta amefeli na kimbilio lake likawa kucheza soka.
"Nilipomaliza shule nikiwa mtaani nacheza soka huku nikiwa dhamira ya kuwa mchezaj mkubwa. Siku moja nikiwa nafanya mazoezi uwanjani kwetu, Babu yangu akaniona na kesho yake akaniita na kuniambia kwamba kama naweza kucheza vizuri mpira then atanipeleka kujiunga na Simba SC ya Dar, yeye aliwahi kuwa mchezaji wa Simba miaka ya nyuma huko, hivyo akanihaidi angenileta Dar nije nijiunge na Simba."
Habari ya kutaka kupelekwa Simba ilimfurahisha sana Juma na hivyo akazidisha juhudi kwenye mazoezi na huku mwenyewe akihangaika kutafuta nauli ya kumuwezesha kwenda Dar kujiunga na Simba.
"Katika harakati za kutafuta nauli ya kuja Dar nikaanza kujishughulisha katika ofisi ya ufundi ya Baba yangu, lakini sikuweza kupata fedha nyingi, hivyo ikabidi niuze viatu vyangu fulani ambavyo kule kwetu tulikuwa tunaviiita SUPRA -nilipouza hivyo viatu kwa shilingi 20,000 nikachanganya na na akiba yangu 5000 jumla nikawa na 25,000 ambayo ilikuwa inanitosha peke yangu kuweza kunifikisha Dar, hivyo nikaamua kuondoka mwenyewe nikiwa na mawazo ya kwenda Simba kuomba mwenyewe.
"Kwa bahati mbaya nilichelewa kukata tiketi hivyo nikazamia kwenye treni. Nilipofika Tabora nikakamatwa na TT na hivyo nikalazimika kulipa nauli na faini kwa kutoa 10,000/=. Kwa kuwa sikuwa na ndugu wala jamaa ninayemfahamu pale Tabora ikabidi nirudi kwenye treni ili niweze kuendelea na safari ya kuja Dar, lakini kwa bahati mbaya fedha niliyobaki nayo haikutosha kunifikisha Dar. TT aliniambia nitaishia Morogoro na hivyo nikalipa shilingi 14,700. Jumatatu tarehe 31 tukafika Morogoro asubuhi nikashushwa na kwa kuwa sikuwa na nauli ikabidi niendelee na safari ya kuja Dar kwa miguu na hatimaye nikafika hapa jijini siku ya Jumanne tarehe 1 na moja kwa moja nikaulizia ilipo klabu ya Simba. Nikaelekezwa na nikafika K'koo nikaenda mpaka pale lakini kwa bahati mbaya nikaambiwa kwamba hakukuwa na mtu kwasababu ilikuwa ni sikukuu. Sikuwa na namna ikabidi niwepo pale pale kariakoo na nikashinda na kulala pale pale. Kesho yake nikapata wazo la kujaribu kuja katika ofisi za Clouds FM ili niweze kuongea na mtu aitwaye Shaffih Dauda ambaye nimekuwa nikimsikia akichambua soka kwenye kipindi cha Sports Extra - ili aweze kunisaidia."
Itaendelea....................................................
MESSI, INIESTA NA RONALDO - NANI KUIBUKA MCHEZAJI BORA WA DUNIA LEO HII???

Unakumbuka nani alikuwa wa pili wakati Iniesta anakuwa mchezaji bora wa Ulaya kwa mwaka 2012? Iniesta hakufuatwa na mtu mmoja nyuma yake, walikuwa wawili nao ni Messi na Cristiano Ronaldo, hawa walikuwa wa pili kwenye tuzo hiyo kwa sababu kura walizopigiwa zililingana. Wakati tukiwa tunangojea kutangazwa kwa mchezaji bora wa dunia baada ya masaa machache, mambo yamebadilika Iniesta bado yupo kwenye kinyang’anyiro hicho lakini si mtu anayepewa nafasi kubwa ya kuwa namba moja tena, nafasi yake ni ya tatu kulingana na na maoni ya wadau wengi, kitu ambacho binafsi naafiki moja kwa moja lakini pia naamini lolote laweza kutokea. Sasa bado utata upo kwenye nani ataishika namba moja?
Basi tuwaangalie Messi, Iniesta na Ronaldo kwa ukaribu katika mwaka 2012;
Messi
Nakuhakikishia asilimia zaidi ya 60 ya watanzania wapenda soka wakiulizwa wao watamchagua nani ashinde tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa sasa, watamchagua huyu, unajua kwa nini? Messi ndiye mwanasoka anayetajwa zaidi kwenye vyombo vya habari kwa hivi sasa hii inatokana na rekodi ambazo amekuwa akizivunja kila kukicha. Rekodi nyingi za ufungaji katika soka sasa zinashikiliwa naye. Tayari Messi ameshashinda tuzo hii mara tatu mfululizo je atafanya hivyo tena kesho? Lolote linawezekana, lakini si watanzania pekee wanaomuona Messi kama ndiye mchezaji bora bali hata vyombo vingi vya habari duniani pia vimekuwa vikimpigia chapuo la kuibuka kidedea.
Iniesta
Kama nilivyosema hapo mwanzo, Iniesta ndiye mchezaji bora wa Ulaya kwa hivi sasa, na ndiye mchezaji bora waligi ya mabingwa Ulaya kwa msimu uliopita na michuano ya kombe la Ulaya kwa mwaka 2012. Iniesta ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu yeye huuchezea mpira vile anavyotaka yeye. Si mfungaji sana lakini ni mtoa pasi za magoli mzuri sana. Iniesta ni moja ya mazao adhimu sana kutoka La Masia, wengine ni Messi na Xavi Hernandes. Je mchezaji bora wa Ulaya atakuwa mchezaji bora wa dunia hapo kesho? Tungoje kidogo tu, kesho si mbali.
Ronaldo
Jose Mourinho, kocha wa Real Madrid aliwahi kusema kuwa kama Messi ni mchezaji bora wa dunia basi Ronaldo ndiye mchezaji bora wa ulimwengu. Kwa mwaka 2012, mambo mengi ya Cristiano yalienda vizuri, yeye alikuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Hispania, La Liga baada ya kuiwezesha Real Madrid kushinda ligi kuu kwa jumla ya pointi 100, pia Ronaldo aliiwezesha Ureno kufika nusu fainali ya kombe la Ulaya huku yeye akiwa ndio mwezeshaji mkuu kufikia mafanikio hayo. Mancini, kocha wa Manchester City alisema wanahitaji polisi kumdhibiti Ronaldo wakati City ilipokuwa ikienda kupambana na Madrid kwenye ligi ya mabingwa Ulaya. Ronaldo pia anapewa nafasi na wachezaji na makocha wengi maarufu. Je Ronaldo atawapiku Messi na Iniesta? Masaa machache tu yamebaki wadau.
By PodoBest
Nifuate twitter: @iPodoBest
Sunday, January 6, 2013
DEMBA BA NI NYOTA NJEMA KWA CHELSEA.

Na PodoBest
Nifwate twitter @iPodoBest
Kuna watu wanadai eti Demba Ba kaondoka Newcastle United kwa sababu anajua muda wake wa kufunga magoli umefikia tamati kwa sasa, Unajua kwa nini wanasema kitu kama hiki? Mpaka kufikia kipindi kama hiki mwaka jana 2012, Ba tayari alikuwa ameshafunga magoli 15 kwenye ligi kuu muda kama huu alisajiliwa Papiss Demba Cisse katika klabu hiyo, Ba alifunga goli moja tu kwenye ligi baada ya Cisse kutua, Hivyo msimu uliisha Ba akiwa kafunga goli 16 tu huku Cisse akifunga goli 13. Najua unajua kilichotokea msimu huu wakati unaanza mpaka mwaka 2012 unaisha ukame wa magoli ulikuwa umehamia kwa Cisse wakati mwenzake, Ba, alikuwa ameshafunga goli 15 mpaka Desemba 31, 2012. Mwaka 2013 umeanza tu na Cisse kaanza kucheka na nyavu kama ilivyokuwa mwaka jana. Sasa hao jamaa wanadai eti Ba anaona hana upepo wa kufunga January mpaka May akiwa na Newcastle ndio maana kaamua kutimka!!
Ha ha ha sasa sahau hizo habari za kina Demba, binafsi nimeuheshimu uamuzi wa Demba Ba kujiunga na Chelsea, kwanza ni uamuzi wa kishujaa, kujiunga sehemu ambayo washambuliaji wakubwa wa dunia wameshindwa kung’aa si uamuzi mdogo. Pili naamini Ba ana nafasi kubwa sana ya kung’aa akiwa na Chelsea kwa sababu ya uwezo wake wa kucheza nafasi za mbele zaidi ya moja. Huyu ndiye aina ya mchezaji ambaye Chelsea ilikuwa ikimhitaji katika kipindi hiki ambacho Didier Drogba hayupo tena katika klabu. Mimi naamini Ba ni moja ya washambuliaji bora kabisa wa wakati huu ndio maana makala yangu ya mwezi wa11 tarehe 16 mwaka jana, ya http://www.shaffihdauda.com/2012/11/wachezaji-20-walioiteka-ulaya-kwa.html “Wachezaji 20 Walioiteka Ulaya Kwa Kuzisaidia Timu Zao” Demba Ba alikuwa wa 18 naamini msimu huu ukiisha Ba atakuwa ndani ya 10 bora kwenye chart kama hii. Hili limeanza kujidhihirisha hapo jana wakati alipofunga goli mbili peke yake wakati Chelsea ilipoishinda goli 5 dhidi ya goli 1 la Southampton kombe la FA. Nyota njema imeonekana asubuhi.
MAZISHI YA KOCHA ALIYEIBUA KIPAJI SHOMARI KAPOMBE YAFANYIKA MOROGORO LEO
Source: http://audifacejackson.blogspot.com
Umati wa watu uliofurika nyumbani kwa marehemu Yahya Mohamed'Berni' jioni hii
Jeneza la marehemu Bern likiswariwa nje ya nyumba yao jioni hii
Vilo vikitawa enei hilo
Mwenyekiti kiti wa CCM mkoa wa Morogoro ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini lnnocent Karogerezi[Wakwanza kushoto akijianda kwenda kuzi maeneo ya Kibwa juu ya Milima ya Uluguru.kwenye shati la draft anaye cheka ni diwani wa Kaya ya Mji Mpya Wencelaus Karogerezi ambaye ni kaka wa damu wa Innocent.
Wananchi wakiingie kwenye gari jeneza la Mzee Berni kwenye gari tayari kwa kueleka kijiji kwao Kibwe juu ua milima ya Uluguru jioni hii
Mchezaji wa zamni wa simba ambaye pia aliwahi kuifundiha timu hiyom na timu ya taifa Taifa Stars Mohamed Msomari mwenye kanzu naye alikuwepo kwenye msiba huo jioni hiio
Kocha maarufu nchini na mchezaji wa zamni wa Reli ya Morogoro na Pan Afrika Ally Jangalu akieleka kuzika kijiji cha kibwe kwa kutumia usafiri wake wa pikipiki jioni hii
Katibu mkuu wa chama cha makocha mkoa wa Morogoro ambaye pia mchezaji wa zamani wa Pamba ya Mwanza Edward Hizza aliyepakizwa akielekea kuzika kwa kutumia boda boda
Bingwa wa disko afrika mashriki na kati Maneno Ngedele'Super Ndegele' ambaye kwa sasa anaishi Afrika kusini naye alinaswa na mtandao huu eneo hilo la Msiba jioni hii,densa huo amekuja mkoan i hapa kula sikuu ya X Mass na Mwaka mpya.
Wachezaji wa timu ya polisi Morogoro ambao kwa sasa wako kambini wakijianda na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom unaotarajia kuanza Januari 26 nao walikuwepo kwenye msiba huo, ikumbukwe wachexaji wengi wa timu ya kikosi cha polisi B kilichoshiriki mshindao ya Uhai hivi karibuni wametoka kwent timu ya Bern
Umati wa watu ukishuhudia jeneza la Mzee Berni likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda kupunzishwa kwenye nyumba yake ya milele
Mtandao huu ulimnasa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Innocent Karogerezi[Wakwanza kushoto] akiteta jambo kwa vicheko na wachezaji wa zamani kwenye msiba huo walioshikana mikono kulini ni mchezji wa zamani wa Tumbaku na Reli ya Morogoro na 'Taifa Stars' John Simkoo na Husein Ngurungu mchezaji wa zamani wa Tumbaku ya Morogoro na Pan Afrika ya Dar es salaama ambaye aliweka rekodi ya kuchea timu ya taifa kwa miaka 12 mfurulizo kwa sasa ni Ngurungu ni dereva wa magari makubwa,anayeangalia kamera ni katibu mkuu wa chma cha soko mkoa wa Morogoro'MRFA' Hamisi Semka
Jeneza la marehemu Bern likiswariwa nje ya nyumba yao jioni hii
Vilo vikitawa enei hilo
Mwenyekiti kiti wa CCM mkoa wa Morogoro ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini lnnocent Karogerezi[Wakwanza kushoto akijianda kwenda kuzi maeneo ya Kibwa juu ya Milima ya Uluguru.kwenye shati la draft anaye cheka ni diwani wa Kaya ya Mji Mpya Wencelaus Karogerezi ambaye ni kaka wa damu wa Innocent.
Wananchi wakiingie kwenye gari jeneza la Mzee Berni kwenye gari tayari kwa kueleka kijiji kwao Kibwe juu ua milima ya Uluguru jioni hii
Mchezaji wa zamni wa simba ambaye pia aliwahi kuifundiha timu hiyom na timu ya taifa Taifa Stars Mohamed Msomari mwenye kanzu naye alikuwepo kwenye msiba huo jioni hiio
Kocha maarufu nchini na mchezaji wa zamni wa Reli ya Morogoro na Pan Afrika Ally Jangalu akieleka kuzika kijiji cha kibwe kwa kutumia usafiri wake wa pikipiki jioni hii
Katibu mkuu wa chama cha makocha mkoa wa Morogoro ambaye pia mchezaji wa zamani wa Pamba ya Mwanza Edward Hizza aliyepakizwa akielekea kuzika kwa kutumia boda boda
Bingwa wa disko afrika mashriki na kati Maneno Ngedele'Super Ndegele' ambaye kwa sasa anaishi Afrika kusini naye alinaswa na mtandao huu eneo hilo la Msiba jioni hii,densa huo amekuja mkoan i hapa kula sikuu ya X Mass na Mwaka mpya.
Wachezaji wa timu ya polisi Morogoro ambao kwa sasa wako kambini wakijianda na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom unaotarajia kuanza Januari 26 nao walikuwepo kwenye msiba huo, ikumbukwe wachexaji wengi wa timu ya kikosi cha polisi B kilichoshiriki mshindao ya Uhai hivi karibuni wametoka kwent timu ya Bern
Umati wa watu ukishuhudia jeneza la Mzee Berni likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda kupunzishwa kwenye nyumba yake ya milele
Mtandao huu ulimnasa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Innocent Karogerezi[Wakwanza kushoto] akiteta jambo kwa vicheko na wachezaji wa zamani kwenye msiba huo walioshikana mikono kulini ni mchezji wa zamani wa Tumbaku na Reli ya Morogoro na 'Taifa Stars' John Simkoo na Husein Ngurungu mchezaji wa zamani wa Tumbaku ya Morogoro na Pan Afrika ya Dar es salaama ambaye aliweka rekodi ya kuchea timu ya taifa kwa miaka 12 mfurulizo kwa sasa ni Ngurungu ni dereva wa magari makubwa,anayeangalia kamera ni katibu mkuu wa chma cha soko mkoa wa Morogoro'MRFA' Hamisi Semka
Saturday, January 5, 2013
YANGA YATOKA SARE NA WATURUKI
Kikosi cha Young Africans kilichoanza leo dhidi ya Armini BielefeldArmini Bielefeld ilianza soka kwa kasi kwa lengo la kujipatia bao la mapema lakini umakini wa walinzi wa Yanga na mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez' ilikuwa kikwazo kwao kwani mashambulizi yao yaliishia mikononi mwake.
Ikiwa ni mchezo wake wa kwanza wa kujipima nguvu Young African iliweza kuonyesha soka safi katika kipindi cha kwanza hali iliyowashangaza wajerumani hao na kipindi cha pili kuamua kufanya mabadiliko ya kikosi kizima.
Viungo wa Yanga Frank Domayo, Haruna Niyonzima na Kabange Twite waliweza kutawala mchezo kwa dakika 45 zote za kipindi cha kwanza huku baadhi ya wajerumani waliokuwa wakishuhudia mchezo huo kushangazwa na kiwango cha timu ya Yanga
Hadi mapumziko timu zote zilikwenda mapumziko , Young Africans 0 - Arminia Bielefeld.
Kipindi cha pili Arminia Bielefeld iliamua kubadilisha kikosi chake chote cha wachezaji kwa lengo la kuingiza nguvu mpya ili waweze kuikabili kasi ya wachezaji wa Yanga ambao walionekana kuwa imara na bora zaidi.
Dakika ya 55 Yanga ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Said Bahanuzi na David Luhende na nafasi zao kuchukuliwa na Jerson Tegete na Saimon Msuva.
Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 60 ya mchezo, akiunganisha pasi safi aliypewa na Saimon Msuva aliyewatoka walinzi wa Arminia Bielefeld na kumpa pasi Tegete ambaye aliukwamisha mpira wavuni na kuhesabu bao la kwanza.
Kuona hivyo wajerumani walikuja juu kusaka bao la kusawazisha, lakini bado ukuta wa Yanga uliendelea kuonekana kuwa makini lakini makosa ya mshika kibendera yaliipelekea Armini Bielefeld kupata bao la kusawazsiha dakika ya 81 kupitia kwa Eric Agyemang amabaye alikua ameotea.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Young Africans 1 - 1 Armini Bielefeld.
Kocha Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema amefurahishwa na kiwango walichokionyesha wachezaji wake na anaamini kadri siku zinavyokwenda wanazidi kuimarika na kuwa bora, hivyo katika michezo mingine wataendelea kuonyesha mabadiliko makubwa.
Young Africans: Ally Mustafa 'Barthez, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani, Kabange Twite, Haruna Niyonzima/Nizar Khalfan, Frank Domayo/Nurdin Bakari, Said Bahanuzi/Jerson Tegete, Didier Kavumbagu, David Luhende/Saimon Msuva - SOURCE: http://youngafricans.co.tz
SIMBA NA TUSKER HAKUNA MBABE MAPINDUZI CUP
TIMU ya soka ya Simba jana ilitoka sare ya bao 1-1 na Tusker ya Kenya
katika mechi ya michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyopigwa kwenye Uwanja
wa Amaan, Zanzibar.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kuanzia saa moja usiku, Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 18 kupitia kwa Haruna Moshi 'Boban' aliyeunganisha wavuni krosi kutoka kwa Ramadhani Chombo 'Redondo'.
Tusker ilisawazisha dakika ya 39 kwa bao lililofungwa na Khalid Aucho na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Licha ya kila timu kufanya mabadiliko kipindi cha pili na pia kushambuliana kwa zamu, hakuna iliyoweza kuongeza bao na hivyo kuzifanya zigawane pointi moja kila moja.
Kwa matokeo hayo, Tusker inaongoza kundi hilo kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, kufuatia kila moja kuwa na pointi tatu baada ya kucheza mechi mbili.
Hii ni mara ya pili kwa Simba kukutana na Tusker katika muda wa wiki moja. Katika mechi ya kirafiki kati ya timu hizo iliyochezwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ilichapwa mabao 3-0 na Tusker.
Katika mechi iliyochezwa jioni, Jamhuri ya Pemba iliichapa Bandari mabao 2-1.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kuanzia saa moja usiku, Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 18 kupitia kwa Haruna Moshi 'Boban' aliyeunganisha wavuni krosi kutoka kwa Ramadhani Chombo 'Redondo'.
Tusker ilisawazisha dakika ya 39 kwa bao lililofungwa na Khalid Aucho na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Licha ya kila timu kufanya mabadiliko kipindi cha pili na pia kushambuliana kwa zamu, hakuna iliyoweza kuongeza bao na hivyo kuzifanya zigawane pointi moja kila moja.
Kwa matokeo hayo, Tusker inaongoza kundi hilo kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, kufuatia kila moja kuwa na pointi tatu baada ya kucheza mechi mbili.
Hii ni mara ya pili kwa Simba kukutana na Tusker katika muda wa wiki moja. Katika mechi ya kirafiki kati ya timu hizo iliyochezwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ilichapwa mabao 3-0 na Tusker.
Katika mechi iliyochezwa jioni, Jamhuri ya Pemba iliichapa Bandari mabao 2-1.
IMETOSHA SASA - KITENDO CHA BOATENG KUTOKA NJE UWANJA - NI HATUA MUHIMU KATIKA VITA DHIDI YA UBAGUZI WA RANGI
Akisapotiwa na nahodha wake Massimo Ambrosini na kufuatiwa na wachezaji wenzake, mchezaji wa Milan Kevin-Prince Boateng aliondoka uwanjani, na kuifanya mechi ya kirafiki kati ya Milan vs Pro Patria kuishia kwenye dakika ya 26.
Yeye na wachezaji wenzie weusi, Urby Emanuelson, Sulley Muntari na M'Baye Niang, walikuwa wakiandamwa vitendo vya kibaguzi kutoka kwenye sehemu mojawapo ya uwanja wa Carlo Speroni. Milan walijaribu kuisimamisha mechi mwanzoni, wakimwambia refa kuchukua maamuzi lakini ilishindikana.
Miongo miwili iliyopita, Gullit alichoswa na matusi ya kibaguzi aliyokuwa akipokea. Milan walimsapoti wakati huo kama walivyofanya kwa Boateng sasa hivi. Timu ilitoka nje ya uwanja kabla ya mchezo kuanza na bango lilosomeka 'Sema hapana kwa ubaguzi wa rangi'. Raisi Silvio Berlusconi alitaka wabaguzi wafungiwe maisha kwenye viwanja vya soka vya Italia na badala ya kuwafanyia sinema ya kuwaruhusu kuingia uwanjani chini uangalizi maalum wa mamlaka husika.
Wakati huo, sapoti ya Milan juu ya vita dhidi ya ubaguzi, ilikuwa ndio mwanzo wa kuvutia jicho la UEFA katika kuliangalia suala hili kwa umakini kwamba lilikuwa tatizo. Lakini suala hili lilishawahi kushughulikiwa katika njia sahihi? Hapana ndio jibu.
Labda kidogo wanaweza kujitetea, baada ya hatua fulani kuchukuliwa na shirikisho la soka nchini Italia (FIGC), Lega Calcio na kamati ya Olympiki ya Italia kufuatia tukio lilotokea kwa Mario Balotelli na Samuel Eto'o katika mechi kati ya Inter vs Cagliari mwezi September, 20, 2009. Tangu wakati, waamuzi wa mechi wana mamlaka yaliyotajwa katika kifungu namba 62, kipengele namba 6 katika sheria ya FIGC ya kusimamisha mechi ikiwa wataona mabango ya kibaguzi au watasikia maneno ya kibaguzi. Lakini kwa sheria hiyo haikuwa mpaka Alhamisi ya juzi (na tena ni Boateng na Ambrosini walioanza kuitumia wakati refa Gianluca Benassi akipotezea), ushahidi wa matendo unatoa hisia kwamba hakuna chombo cha maamuzi kilichopigana vita ya ubaguzi wa rangi katika hali ya kuridhisha kabisa.
Kama wameshindwa kuchukua maamuzi muhimu dhid ya vita hii, basi wachezaji wenyewe watachukua hatua mikononi mwao - angalia namna kitendo cha Boateng cha kupingana na ubaguzi kilivyopokelewa vizuri na kushangiliwa kwa wingi na asilimia kubwa ya washabiki waliojaza katika uwanja wa Carlo Speroni. Ilikuwa hatua muhimu. Kocha wa Italy Cesare Prandelli aliguswa na kitendo cha Boateng na akaongea. "Hatimaye, inachosa, inakera na haya ndio matokeo yake."
Prandelli amefanya kazi nzuri katika kuleta mchanganyiko wa rangi kwa wachezaji wake wa timu ya taifa, akiwachagua Angelo Ogbonna, Balotelli na Stephan El Shaarawy, wachezaji wachanga ambao anawatengeneza kuwa future ya soka la Italia. Japo wachache lakini hayupo mbali.
"Italia inahitaji na raia wastaraabu na wenye upeo kiasi," kocha wa Milan Massimiliano Allegri aliviambia vyombo vya habari. "Natumai hii itakuwa ishara muhimu ya kufuatwa kutoka kwenye ligi za chini mpaka kwenye Serie A."
Je mambo yatakuwa tofauti ikiwa tukio kama hilo litatokea tena? Milan wanasisitiza kuusimamsiha mchezo ndio njia watakayofuata sasa. "Tunahitaji uvumilivu sifuri kwenye matukio kama haya," anasema mwanachama wa bodi Barbara Berlusconi, "Na michezo inabidi isimamishwe hata kwenye Serie A sio mechi za kirafiki tu." Niang, mmoja ya watu waliokumbwa na tukio la Alhamisi, pia amesema Milan watakuwa tayari kufanya kitendo cha kugomea mchezo tena ikiwa tukio la kibaguzi litatokea kwenye mechi yao - hata katika mechi yao dhidi ya Barcelona mwezi ujao.
Hilo linabaki kusubiriwa kuonekana kama litatokea, lakini katika mechi ya ushindani au kirafiki, Boateng amechukua hatua muhimu katika vita dhidi ya ubaguzi kwa kutoka uwanjani na wachezaji wenzake - ni hatua muhimu katika kupambana na tatizo hili.
Sio wote wanaokubaliana na suala la Boateng. Mchezaji wa zamani wa Milan Clerence Seerdorf aliiambia BBC: "Sidhani kama ni kitu kizuri. Hawa wabaguzi watajisikia kuwa na nguvu sasa. Wanatakiwa kutambulika na kuondolewa katika uwanja." Pia Seedorf amepata mtu anayetetea hoja yake akisema uondoaji wa ubaguzi kwenye soka utakuja kupitia elimu akisema "Hakuna anayezaliwa mbaguzi, wanakuwa hivyo baada ya kuishi.' - mchezaji wa zamani wa Juventus Lilian Thuram, lakini pia anasisitiza kwa kitendo cha Milan kutoka nje ya uwanja ni hatua muhimu katika vita dhidi ya ubaguzi.
Akiwa kocha wa Valencia katika miaka ya 90, Guus Hiddink, ambaye baba yake alikuwa kwenye jeshi la Uholanzi lilopigana vita ya pili ya dunia dhidi ya Hitler, aliona bango lenye alama ya NAZI jukwaani, akasisitiza kama halitokuwa limetolewa kabla ya mchezo kuanza, timu yake haitocheza, na ikiwa litaondolewa na likawekwa baada ya mchezo kuanza then angeiongoza timu yake kutoka nje ya uwanja.
Stuttgart pia waliwahi kumfukuza mchezaji kwa tuhuma za ubaguzi wa rangi mwaka 1999. Baada ya kumbagua mchezaji mwenzie kwa kuweka bango lenye maneno ya kibaguzi kwenye chumba cha kufanyia mazoezi ya viungo.
Hivyo wapo watu waliokuwa wanapigana na vita hii ya ubaguzi wa rangi kwenye soka tangu zamani. Lakini inawezekana walipotezewa au hawakuwa wanaandikwa kwenye vyombo vya habari, au wamesahaulika. Kutoka nje ya uwanja kwa Boateng na timu yake ya Milan kumetengeneza vichwa vya habari duniani, na La Gazzetta dello Sport wamelichukuliwa suala la alhamisi iliyopita kwa umakini mkubwa - kuna makala imeanzishwa inaitwa: "Sisi wote ni Boateng," ambayo inasema "Sisi ni weusi kama Boateng. Kitendo hichi kinaonyesha mshikamano unaotakiwa kuwepo kama ilivyokuwa kwa wachezaji wa Treviso walipopaka sura zao rangi nyeusi kuonyesha sapoti kwa mchezaji mwenzao wa kinigeria Omolade Akeem baada ya kutukanwa kibaguzi na mashabiki wa timu yake mwenyewe mwaka 2001.
Lakini story kama hiyo haikupata kuwekwa kwenye ukurasa wa mbele, kama suala la kutoka nje kwa Boateng na Milan halikupewa nguvu ya kutosha kwenye vyombo vya habari vingine kama walivyolipa kipaumbele suala la ugomvi Mario Balotelli na Roberto Mancini - japokuwa mwisho wa siku ni biashara hivyo wanaweza kueleweka. Ingawa suala la Boateng na Milan lilikuwa lina maana kwa jamii kuliko ishu ya kichaa Balotelli na baba yake Mancini. Suala la Boateng linaweza likaleta mabadiliko na kuhamsisha vita dhdi ya ubaguzi wa rangi.
Kwa kitendo walichofanya Milan sasa inabidi Platini na UEFA yake wachukue hatua zinazoridhisha juu ya vita dhdi ya ubaguzi wa rangi - asante kwa Milan kwa kuanzisha njia mpya ya kuelekea kwenye ukombozi wa wachezaji weusi - "Bravo, Boateng. Bravo, Milan.
Subscribe to:
Posts (Atom)









