Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa fainali za mataifa huru ya Afrika huko nchini Afrika ya Kusini, mchezaji bora wa bara la Afrika Yaya Toure ameugua ghafla kifua na homa kali na sasa amelazwa katika hospitali moja huko Abu Dhabi walipoweka kambi na timu yake ya taifa ya Ivory Coast.
Kikosi cha Ivory Coast kiliwasili UAE siku ya jumamosi wakitokea Paris, wakati timu ilipokutana na maofisa wengine kabla ya kwenda Uarabuni.
Toure hakuwepo kwenye mazoezi ya kawaida ya timu hiyo siku ya jumapili, wakati maofisa wa afya wa timu hiyo wakijaribu kufanya kazi ya ziada kuweza kuirejesha hali ya mchezaji kwenye usawa huku wakishindwa kusema ni lini atarudi mazoezini.
Nahodha wa timu hiyo Didier Drogba pia hakuweza kufanya mazoezi jana kwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya kichwa.
Ivory Coast watacheza mechi ya kirafiki na Egypt January 14 kabla ya kusafiri kwenda South Africa siku mbili baadae kwa ajili ya AFCON 2012.
No comments:
Post a Comment