Search This Blog

Monday, January 7, 2013

OMARY 'MWAMBA ' KAPERA -RAISI KIKWETE TUKUMBUKE HATA SISI WANAMICHEZO WA ZAMANI

Beki wa zamani wa vilabu vya Yanga,Pan African na Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Omary ‘Mwamba ‘ Kapera ameiomba Serikali kuwaangalia kwa ukaribu wanamichezo wa zamani ambao kwasasa wanasumbuliwa na maradhi mbali mbali walioliletea sifa Taifa letu kupitia michezo hasa mchezo wa soka. Kapera ambaye kwasasa anasumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi pia amemuomba Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete na Serikali yake kutafuta namna ya kuwasaidia wanamichezo wa zamani.
                     Huyu ndo Mwamba Kapera enzi zake....

Hapa namnukuu Kapera ‘’Nilipata Stroke ya mwili nikaanguka lakini bahati nzuri nimejitibu kwa kushirikiana na watoto wangu walau nimepata nafuu,lakini bado sijapona kabisa na hilo ndilo tatizo kubwa linalonikabili kwasasa,na katika kipindi chote cha kuugua nimekuwa nikipata msaada mkubwa kutoka kwa watoto lakini sipati msaada kutoka Serikani,silazimishi lakini kati ya watu wanaoangaliwa kwa ukaribu na serikali basi nasisi wachezaji wa zamani tuangaliwe’’. Omary Kapera alikuwa Sentahafu maarufu wa vilabu vya Yanga,Pan African na timu ya Taifa alikuwa maarufu kwa jina la ‘Mwamba’ kutokana na umahili wake wa kuwazuia washambuliaji wakali kama Willy Mwaijibe,Adam Sabu na Khalid Abeid. Mwamba Kapera aliendelea kunena yafuatayo,’‘Raisi Kikwete juzi juzi amewatunuku wasanii kina Muhidini Gurumo na Bi Kidude tunashukuru amefanya vizuri lakini arudi na kwa wachezaji na sisi tufarijike kwa namna moja ama nyingine,ni hilo tu’’

    Hivi ndivyo Mwamba Kapera alivyo hivi sasa.....hapa nilimtembelea nyumbani kwake.

Kama ningepata nafasi ya kukutana ana kwa ana na Raisi Kikwete ningemwambia atuangalie wachezaji wazamani tunaoumwa na hata wale wazima,atuangalie kwa ukaribu kwani hali zetu siyo nzuri,kutuangalia haina maana kwamba Raisi Kikwete ndiye atuangalie, hapan yeye atoe amri,akitoa amri wapo watu watakaofanya iyo kazi kwa niaba yake’ Kapera pia amesema hana sababu ya kukumbuka mema aliyofanya akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania, ‘‘

'' Nimeichezea timu ya Taifa kwa muda mrefu lakini haaa! siikumbuki kwasababu na wao hawanikumbuki namimi siikumbuki,Yanga ni kama Nyumbani nimeichezea Yanga kwa kipindi cha miaka kumi,nimelelewa na YANGA,Yanga imenifanya nimetembee duniani kote,sikupata kitu lakini nilijitangaza na umaarufu wangu wote niliupata kwasababu ya Yanga kwaiyo nina haki ya Kuisemea ‘’

2 comments:

  1. ndivyo inavyotakiwa ni lazima Serikali iwaangalie wachezajiwetu wa zamani ni kweli walileta sifa sana kwa mpira wa Tanzania

    ReplyDelete
  2. NI MUHIMU WAKAANGALIWA NA SERIKALI.KWANI HAWA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA WA ZAMANI WALITUMIKIA TAIFA KWA UADILIFU.AIDHA NASHAURI WAUNDE UMOJA WAO UTAKAO WASAIDIA KWENYE SHIDA NA RAHA.MBONA WAZEE WALIOPIGANA VITA KUU YA PILI YA DUNIA WANA UMMOJA WAO?

    ReplyDelete