Timu
ya Young Africans Sports Club kesho itashuka dimbani kucheza na timu
ya Denizlispor FC ya ligi daraja la kwanza nchini Uturuki katika mchezo
wa kirafiki utakaofanyika katika uwanja wa Selen Football -Kalimya
Complex pembeni kidogo ya mji wa Antlaya.
Young Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo
jijini Antalya itatumia mchezo huo kama fursa ya kujipima nguvu na timu
hiyo la Denizlispor FC ambayo imeshuka kutoka ligi kuu ya Uturuki mwaka
jana na hivi sasa inapamabana kurudi tena katika Ligi Kuu ya Uturuki.
Kocha
Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kupata
nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Denizlispor FC ambayo ina
wachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo anaamini utakua ni mchezo safi
na kuwavutia.
Baada ya kuwa na
wiki moja ya mazoezi na mechi moja ya kirafiki dhidi ya Armini Bielefeld
ya ujerumani mwishoni mwa wiki itakua ni fursa nyingine nzuri ya
kucheza mchezo wa kirafiki na timu nyingine, hii itanisadia kuona
maendeleo ya kikosi changu kutokana na mazoezi ambayo tumekuwa
tukiyafanya tangu tulipofika alisema 'Brandts'
Denizlispor
FC ni miongoni mwa timu zaidi ya 200 kutoka shemu tofauti duniani
ambazo zimeweka kambi katika mji wa Antlaya kwa ajili ya maandilizi ya
mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la kwanza nchini Uturuki.
Mchezaji
wa zamani wa Leicester City ya Uingereza, Dundee United ya Scotland na
Ivernes ya Uholanzi, mtanzania mzaliwa wa Uingereza Eric Odhiambo ni
miongoni mwa washambuliaji wa kutegemewa wa timu ya Denizlispor FC.
Young
Africans imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari
kabisa kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa kesho katika uwanja wa Selen
Football - Kalimya complex pemebeni kidogo ya mji wa Antalya.
Kikosi
cha wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na
hakuna maheruhi hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia
mchezaji yoyote katika mchezo huo.
Athumani Idd
'Chuji' na Hamis Kiiza waliokuwa wakijisikia vibaya kabla ya mchezo wa
juzi dhidi ya Amrnini Bielefeld wanaendelea vizrui kabisa kwani
wanaendelea na mazoezi pamoja na wachezaji wengine waliopo na timu mjini
Antalya.
Kuhusu hali ya hewa leo haijaonekana
kuwa tatizo kwa wachezaji kwani wanaonekana kuimudu na mda mwingi kwa
sasa kumekua na jua linalowaka kuanzia asubuhu wakati wa mazoezi mpaka
mida ya jioni, kwa leo hali ya hewa ni nyuzi joto 17 - 21, hivyo hali ya
hewa ni nzuri kabisa na jua linawaka mda wote.
SOURCE:youngafrican.co.tz
No comments:
Post a Comment