Search This Blog

Monday, January 7, 2013

JUMA OMARY- ' NILIUZA SUPRA ZANGU ILI NIPATE NAULI YA KUJA DAR KUCHEZA SOKA'




Katika sehemu ya kwanza ya story hii ya kijana wa kitanzania kutoka mkoani Katavi Juma Karim Omary akielezea namna alivyokuwa akitafuta njia ya kuweza kufanikiwa kisoka akiwa mkoani kwao baada ya kufeli kimasomo, hivyo akaamua kudhamiria kujituma ili mpira uweze kuwa ajira yake. Sehemu ya pili ya stori tutaona namna kijana huyo alivyoweza kusafiri kutoka Katavi mpaka kufika Dar es Salaam.

Juma anasema sio kwamba hakuwa anapenda shule kama apendavyo soka, bali kulitokea matatizo wakati akifanya mitihani yake ya kumaliza elimu ya sekondari hivyo akajikuta amefeli na kimbilio lake likawa kucheza soka.

"Nilipomaliza shule nikiwa mtaani nacheza soka huku nikiwa dhamira ya kuwa mchezaj mkubwa. Siku moja nikiwa nafanya mazoezi uwanjani kwetu, Babu yangu akaniona na kesho yake akaniita na kuniambia kwamba kama naweza kucheza vizuri mpira then atanipeleka kujiunga na Simba SC ya Dar, yeye aliwahi kuwa mchezaji wa Simba miaka ya nyuma huko, hivyo akanihaidi angenileta Dar nije nijiunge na Simba."

Habari ya kutaka kupelekwa Simba ilimfurahisha sana Juma na hivyo akazidisha juhudi kwenye mazoezi na huku mwenyewe akihangaika kutafuta nauli ya kumuwezesha kwenda Dar kujiunga na Simba.

"Katika harakati za kutafuta nauli ya kuja Dar nikaanza kujishughulisha katika ofisi ya ufundi ya Baba yangu, lakini sikuweza kupata fedha nyingi, hivyo ikabidi niuze viatu vyangu fulani ambavyo kule kwetu tulikuwa tunaviiita SUPRA -nilipouza hivyo viatu kwa shilingi 20,000 nikachanganya na na akiba yangu 5000 jumla nikawa na 25,000 ambayo ilikuwa inanitosha peke yangu kuweza kunifikisha Dar, hivyo nikaamua kuondoka mwenyewe nikiwa na mawazo ya kwenda Simba kuomba mwenyewe.

"Kwa bahati mbaya nilichelewa kukata tiketi hivyo nikazamia kwenye treni. Nilipofika Tabora nikakamatwa na TT na hivyo nikalazimika kulipa nauli na faini kwa kutoa 10,000/=. Kwa kuwa sikuwa na ndugu wala jamaa ninayemfahamu pale Tabora ikabidi nirudi kwenye treni ili niweze kuendelea na safari ya kuja Dar, lakini kwa bahati mbaya fedha niliyobaki nayo haikutosha kunifikisha Dar. TT aliniambia nitaishia Morogoro na hivyo nikalipa shilingi 14,700. Jumatatu tarehe 31 tukafika Morogoro asubuhi nikashushwa na kwa kuwa sikuwa na nauli ikabidi niendelee na safari ya kuja Dar kwa miguu na hatimaye nikafika hapa jijini siku ya Jumanne tarehe 1 na moja kwa moja nikaulizia ilipo klabu ya Simba. Nikaelekezwa na nikafika K'koo nikaenda mpaka pale lakini kwa bahati mbaya nikaambiwa kwamba hakukuwa na mtu kwasababu ilikuwa ni sikukuu. Sikuwa na namna ikabidi niwepo pale pale kariakoo na nikashinda na kulala pale pale. Kesho yake nikapata wazo la kujaribu kuja katika ofisi za Clouds FM ili niweze kuongea na mtu aitwaye Shaffih Dauda ambaye nimekuwa nikimsikia akichambua soka kwenye kipindi cha Sports Extra - ili aweze kunisaidia."

Itaendelea....................................................

7 comments:

  1. Very interesting.Hatudanganywi kweli?moro mpaka dar kwa miguu,mhhhhhhh

    ReplyDelete
    Replies
    1. ndizi nyama wewe. unashangaa moro. DAR mpaka mwanza watu wanapiga tena siku moja tu akichelewa sana atafika jioni.

      Delete
  2. safi kaka kip it up. kama itawezekana mwonyeshe mwanga dogo.tyson alikuwa mtaani kabisa,akasaidiwa na baadae akaja kuwa mtu maarufu sana kwenye Carrier yake..Baloteli????

    ReplyDelete
  3. mara nyingi mwanzo huwa ni mgumu ila izingatiwe tu kwamba mvumilivu hula mbivu. mungu amsaidie kipaji chake kiyabadilishe maisha yake.

    ReplyDelete
  4. stry kwel nzur ila kipaji kipo kwel hapo??

    ReplyDelete
  5. Namtakia mafanikio mema Juma coz anaonekana yupo serious na mpira...ALL THE BEST

    ReplyDelete
  6. kama anataka kucheza simba atapotea kwanza ajiunge na yanga B atatok. simba B Wanapigasoka balaa tatizo siasa hawalipw wanacheza bure.

    ReplyDelete