Search This Blog

Monday, January 7, 2013

KALI YA LEO: IKER CASILLAS ALIPOKATAA KITAMBAA CHA UNAHODHA KUTOKA KWA CRISTIANO RONALDO

Kama alivyofanya katika mchezo wa mwisho kabla ya mwaka kuisha, Jose Mourinho aliamua kumpiga benchi tena golikipa Iker Casillas katika mchezo wa kufungua mwaka dhidi ya Real Sociedad. Wakati huu, kwa bahati mbaya mambo hayakwenda kama Mourinho alivyotaka.

  Kipa aliyeanza Antonio Adan alionyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya sita, na kumlazimu Mourinho kumuingiza Casillas kwenye mchezo huo. Pmaoja na adhabu ya penati waliyopewa kutoka na faulo aliyofanya Adan, Sociedad walienda na kufunga mara mbili katika kipindi cha kwanza wakichuana vikali na Madrid.
Lakini baada ya penati kupigwa kitu kisicho cha kawaida kikatokea. Cristiano Ronaldo akiwa amevaa kitambaa cha unahodha kwa mara ya kwanza kwenye mechi rasmi ya mashindano, alikivua kitambaa hicho na kwenda kumpeleka Casillas katika dakika ya 12 ya mchezo. Casillas akakataa na kumsukuma Ronaldo, hivyo Ronaldo akakivaa tena kitambaa na kuendelea na mchezo ulioisha kwa 4-3 huku Ronnie akifunga mabao mawili.

5 comments:

  1. Hasira katika mchezo ukijmlisha fitna hazitakiwi kwanini Ronardo akivue kitambaa wakati hakuwa anatoka nje ya uwanja alikuwa anamaanisha nini kama sio ukorofi

    ReplyDelete
  2. Heshima ktk mchezo wa Soka, hata kama yuko uwanjani ikiwa captain anayetambulika alikuwa nje na kuingia uwanjani, yule asst wake anapaswa kukabidhi kitambaa. Tumeona hata kwa Chelsea Petr anapokuwa amevaa kitambaa wakati Lampard akiwa nje ya uwanja, akiingia uwanjani Petr huwapatia wachezaji wanzake kitambaa wampelekee. Its normal sijaona kosa la Ronaldo.

    ReplyDelete
  3. CJAONA KOSA LA RONALDO IZO NI ILA ZA CASILAS.RONALDO KARIBU UTD

    ReplyDelete
  4. na waunga mkno wote ronaldo kaonyesha ukomavu na nidhamu ktk mchezo kwa kumheshimu capt wake, ila labda tusiende mbele sana yawezekana labda bwana iker cassilas alimtaka tu kimchezo aendelee kuwa nahodha kwa mchezo huo kwa kumsukuma na kumtania sisi tukaona labda kamaind ila wenyewe wanajuana bwana

    ReplyDelete