Na PodoBest
Nifwate twitter @iPodoBest
Kuna watu wanadai eti Demba Ba kaondoka Newcastle United kwa sababu anajua muda wake wa kufunga magoli umefikia tamati kwa sasa, Unajua kwa nini wanasema kitu kama hiki? Mpaka kufikia kipindi kama hiki mwaka jana 2012, Ba tayari alikuwa ameshafunga magoli 15 kwenye ligi kuu muda kama huu alisajiliwa Papiss Demba Cisse katika klabu hiyo, Ba alifunga goli moja tu kwenye ligi baada ya Cisse kutua, Hivyo msimu uliisha Ba akiwa kafunga goli 16 tu huku Cisse akifunga goli 13. Najua unajua kilichotokea msimu huu wakati unaanza mpaka mwaka 2012 unaisha ukame wa magoli ulikuwa umehamia kwa Cisse wakati mwenzake, Ba, alikuwa ameshafunga goli 15 mpaka Desemba 31, 2012. Mwaka 2013 umeanza tu na Cisse kaanza kucheka na nyavu kama ilivyokuwa mwaka jana. Sasa hao jamaa wanadai eti Ba anaona hana upepo wa kufunga January mpaka May akiwa na Newcastle ndio maana kaamua kutimka!!
Ha ha ha sasa sahau hizo habari za kina Demba, binafsi nimeuheshimu uamuzi wa Demba Ba kujiunga na Chelsea, kwanza ni uamuzi wa kishujaa, kujiunga sehemu ambayo washambuliaji wakubwa wa dunia wameshindwa kung’aa si uamuzi mdogo. Pili naamini Ba ana nafasi kubwa sana ya kung’aa akiwa na Chelsea kwa sababu ya uwezo wake wa kucheza nafasi za mbele zaidi ya moja. Huyu ndiye aina ya mchezaji ambaye Chelsea ilikuwa ikimhitaji katika kipindi hiki ambacho Didier Drogba hayupo tena katika klabu. Mimi naamini Ba ni moja ya washambuliaji bora kabisa wa wakati huu ndio maana makala yangu ya mwezi wa11 tarehe 16 mwaka jana, ya http://www.shaffihdauda.com/2012/11/wachezaji-20-walioiteka-ulaya-kwa.html “Wachezaji 20 Walioiteka Ulaya Kwa Kuzisaidia Timu Zao” Demba Ba alikuwa wa 18 naamini msimu huu ukiisha Ba atakuwa ndani ya 10 bora kwenye chart kama hii. Hili limeanza kujidhihirisha hapo jana wakati alipofunga goli mbili peke yake wakati Chelsea ilipoishinda goli 5 dhidi ya goli 1 la Southampton kombe la FA. Nyota njema imeonekana asubuhi.
hapo umesema neno shafii. naamini chelsea itabadilika kwa ujio wake,pia sasa tutaona ufundi wa mata,oscar na harzad kumtengenezea mipara. end of torres is sasa.
ReplyDeletewille namanga
nilikuwa sins wasiwasi nilivyosikia kwamba ba atatua chelsea, nikajua sasa tumondokana na matatizo yanayotusibu sisi chelsea. maana tulikuwa tunacheza bila mtu mbele, unamshangaa tores anavyojificha kwenye matukio na kuanguka muda muhimu. chelsea stiker miaka yote ni watu weusi.....
ReplyDeleteMwanjala, wa Mwanza