Search This Blog

Saturday, January 5, 2013

IMETOSHA SASA - KITENDO CHA BOATENG KUTOKA NJE UWANJA - NI HATUA MUHIMU KATIKA VITA DHIDI YA UBAGUZI WA RANGI

Imetosha sasa.

Akisapotiwa na nahodha wake Massimo Ambrosini na kufuatiwa na wachezaji wenzake, mchezaji wa Milan Kevin-Prince Boateng aliondoka uwanjani, na kuifanya mechi ya kirafiki kati ya Milan vs Pro Patria kuishia kwenye dakika ya 26.

Yeye na wachezaji wenzie weusi, Urby Emanuelson, Sulley Muntari na M'Baye Niang, walikuwa wakiandamwa vitendo vya kibaguzi kutoka kwenye sehemu mojawapo ya uwanja wa Carlo Speroni. Milan walijaribu kuisimamisha mechi mwanzoni, wakimwambia refa kuchukua maamuzi lakini ilishindikana.



Akionekana kukasirishwa sana, Boateng alichukua maamuzi mwenyewe, akabeba mpira na kuubutua kwenye mabango ambayo yalikuwa ndio uzio wa uwanja kutoka kwa mashabiki na uwanja, kabla haujachukua mpira huo na kuanza kuondoka.

Miongo miwili iliyopita, Gullit alichoswa na matusi ya kibaguzi aliyokuwa akipokea. Milan walimsapoti wakati huo kama walivyofanya kwa Boateng sasa hivi. Timu ilitoka nje ya uwanja kabla ya mchezo kuanza na bango lilosomeka 'Sema hapana kwa ubaguzi wa rangi'. Raisi Silvio Berlusconi alitaka wabaguzi wafungiwe maisha kwenye viwanja vya soka vya Italia na badala ya kuwafanyia sinema ya kuwaruhusu kuingia uwanjani chini uangalizi maalum wa mamlaka husika.


Wakati huo, sapoti ya Milan juu ya vita dhidi ya ubaguzi, ilikuwa ndio mwanzo wa kuvutia jicho la UEFA katika kuliangalia suala hili kwa umakini kwamba lilikuwa tatizo. Lakini suala hili lilishawahi kushughulikiwa katika njia sahihi? Hapana ndio jibu.

Labda kidogo wanaweza kujitetea, baada ya hatua fulani kuchukuliwa na shirikisho la soka nchini Italia (FIGC), Lega Calcio na kamati ya Olympiki ya Italia kufuatia tukio lilotokea kwa Mario Balotelli na Samuel Eto'o katika mechi kati ya Inter vs Cagliari mwezi September, 20, 2009. Tangu wakati, waamuzi wa mechi wana mamlaka yaliyotajwa katika kifungu namba 62, kipengele namba 6 katika sheria ya FIGC ya kusimamisha mechi ikiwa wataona mabango ya kibaguzi au watasikia maneno ya kibaguzi. Lakini kwa sheria hiyo haikuwa mpaka Alhamisi ya juzi (na tena ni Boateng na Ambrosini walioanza kuitumia wakati refa Gianluca Benassi akipotezea), ushahidi wa matendo unatoa hisia kwamba hakuna chombo cha maamuzi kilichopigana vita ya ubaguzi wa rangi katika hali ya kuridhisha kabisa.

Kama wameshindwa kuchukua maamuzi muhimu dhid ya vita hii, basi wachezaji wenyewe watachukua hatua mikononi mwao - angalia namna kitendo cha Boateng cha kupingana na ubaguzi kilivyopokelewa vizuri na kushangiliwa kwa wingi na asilimia kubwa ya washabiki waliojaza katika uwanja wa Carlo Speroni. Ilikuwa hatua muhimu. Kocha wa Italy Cesare Prandelli aliguswa na kitendo cha Boateng na akaongea. "Hatimaye, inachosa, inakera na haya ndio matokeo yake."

Prandelli amefanya kazi nzuri katika kuleta mchanganyiko wa rangi kwa wachezaji wake wa timu ya taifa, akiwachagua Angelo Ogbonna, Balotelli na Stephan El Shaarawy, wachezaji wachanga ambao anawatengeneza kuwa future ya soka la Italia. Japo wachache lakini hayupo mbali.

"Italia inahitaji na raia wastaraabu na wenye upeo kiasi," kocha wa Milan Massimiliano Allegri aliviambia vyombo vya habari. "Natumai hii itakuwa ishara muhimu ya kufuatwa kutoka kwenye ligi za chini mpaka kwenye Serie A."

Je mambo yatakuwa tofauti ikiwa tukio kama hilo litatokea tena? Milan wanasisitiza kuusimamsiha mchezo ndio njia watakayofuata sasa. "Tunahitaji uvumilivu sifuri  kwenye matukio kama haya," anasema mwanachama wa bodi Barbara Berlusconi, "Na michezo inabidi isimamishwe hata kwenye Serie A sio mechi za kirafiki tu." Niang, mmoja ya watu waliokumbwa na tukio la Alhamisi, pia amesema Milan watakuwa tayari kufanya kitendo cha kugomea mchezo tena ikiwa tukio la kibaguzi litatokea kwenye mechi yao - hata katika mechi yao dhidi ya Barcelona mwezi ujao.

Hilo linabaki kusubiriwa kuonekana kama litatokea, lakini katika mechi ya ushindani au kirafiki, Boateng amechukua hatua muhimu katika vita dhidi ya ubaguzi kwa kutoka uwanjani na wachezaji wenzake - ni hatua muhimu katika kupambana na tatizo hili.

Sio wote wanaokubaliana na suala la Boateng. Mchezaji wa zamani wa Milan Clerence Seerdorf  aliiambia BBC: "Sidhani kama ni kitu kizuri. Hawa wabaguzi watajisikia kuwa na nguvu sasa. Wanatakiwa kutambulika na kuondolewa katika uwanja." Pia Seedorf amepata mtu anayetetea hoja yake akisema uondoaji wa ubaguzi kwenye soka utakuja kupitia elimu akisema "Hakuna anayezaliwa mbaguzi, wanakuwa hivyo baada ya kuishi.' - mchezaji wa zamani wa Juventus Lilian Thuram, lakini pia anasisitiza kwa kitendo cha Milan kutoka nje ya uwanja ni hatua muhimu katika vita dhidi ya ubaguzi.

Akiwa kocha wa Valencia katika miaka ya 90, Guus Hiddink, ambaye baba yake alikuwa kwenye jeshi la Uholanzi lilopigana vita ya pili ya dunia dhidi ya Hitler, aliona bango lenye alama ya NAZI jukwaani, akasisitiza kama halitokuwa limetolewa kabla ya mchezo kuanza, timu yake haitocheza, na ikiwa litaondolewa na likawekwa baada ya mchezo kuanza then angeiongoza timu yake kutoka nje ya uwanja.

Stuttgart pia waliwahi kumfukuza mchezaji kwa tuhuma za ubaguzi wa rangi mwaka 1999. Baada ya kumbagua mchezaji mwenzie kwa kuweka bango lenye maneno ya kibaguzi kwenye chumba cha kufanyia mazoezi ya viungo.

Hivyo wapo watu waliokuwa wanapigana na vita hii ya ubaguzi wa rangi kwenye soka tangu zamani. Lakini inawezekana walipotezewa au hawakuwa wanaandikwa kwenye vyombo vya habari, au wamesahaulika. Kutoka nje ya uwanja kwa Boateng na timu yake ya Milan kumetengeneza vichwa vya habari duniani, na  La Gazzetta dello Sport wamelichukuliwa suala la alhamisi iliyopita kwa umakini mkubwa - kuna makala imeanzishwa inaitwa: "Sisi wote ni Boateng," ambayo inasema "Sisi ni weusi kama Boateng. Kitendo hichi kinaonyesha mshikamano unaotakiwa kuwepo kama ilivyokuwa kwa wachezaji wa Treviso walipopaka sura zao rangi nyeusi kuonyesha sapoti kwa mchezaji mwenzao wa kinigeria Omolade Akeem baada ya kutukanwa kibaguzi na mashabiki wa timu yake mwenyewe mwaka 2001.

Lakini story kama hiyo haikupata kuwekwa kwenye ukurasa wa mbele, kama suala la kutoka nje kwa Boateng na Milan halikupewa nguvu ya kutosha kwenye vyombo vya habari vingine kama walivyolipa kipaumbele suala la ugomvi Mario Balotelli  na Roberto Mancini - japokuwa mwisho wa siku ni biashara hivyo wanaweza kueleweka. Ingawa suala la Boateng na Milan lilikuwa lina maana kwa jamii kuliko ishu ya kichaa Balotelli na baba yake Mancini. Suala la Boateng linaweza likaleta mabadiliko na kuhamsisha vita dhdi ya ubaguzi wa rangi. 

Kwa kitendo walichofanya Milan sasa inabidi Platini na UEFA yake wachukue hatua zinazoridhisha juu ya vita dhdi ya ubaguzi wa rangi - asante kwa Milan kwa kuanzisha njia mpya ya kuelekea kwenye ukombozi wa wachezaji weusi - "Bravo, Boateng. Bravo, Milan.

No comments:

Post a Comment