Search This Blog

Friday, January 4, 2013

ATHUMANI KILAMBO- ' NAOMBENI MSAADA NASUMBULIWA NA UGONJWA WA KANSA YA KOO '

Kocha na mwanzilishi wa Pan African ya jijini Dar Es Salaam Kilambo Athumani  anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya koo,
‘ nasumbuliwa na kansa ya koo takribani miaka miwili sasa,nimekuwa nikija hapa mara kwa mara kwa ajili ya kupoza makali tu’ hayo ni maneno ya Kilambo mara baada ya kupewa ruhusa ya kuondoka kwenye hospitali ya Ocean Road ya jijini Dar Es Salaam hii leo,
Kilambo amewaomba wadau wa michezo mbali mbali kujitokeza kwa wingi na kumsaidia hasa katika kipindi hiki kigumu kumchangia kwa hali na mali ili aweze kutibiwa ugonjwa huu unaomsumbua na kuhatarisha maisha yake kwa muda sasa,
‘ Wakati Pan African tunaianzisha mnamo mwaka 1976 lengo kubwa lilikua ni kuanzisha klabu kwa ajili ya kusaidiana wakati wa shida na raha,suala la kuianzisha timu ya mpira lilikuja baadae,wakati ule umoja wetu ulikua na nguvu sana kiasi kwamba wakati wa matatizo na raha tulikuwa sote,sasa nawaomba wadau wa michezo hasa wachezaji wa zamani kukumbuka enzi zetu  kwa kusaidiana pia kipindi hiki ’ alimalizia kusema ndugu Kilambo.
Miongoni mwa waanzilishi wa klabu ya PAN AFRICAN ni mkurugenzi  mtendaji  wa mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii wa NSSF,Dr Ramadhani Dau, marehemu Sam Dee,Mzee Ally Abbas,Shiraz Sharrif,Mzee Paul Sozigwa, Dr William Ugundo na wengineo wengi
Baadhi ya wachezaji waanzilishi wa Pan African  ni Omary Kapera,Adolf Rishard,Jellah Mtagwa, Mohamed Mkweche,Sunday Manara na Kitwana Manara,Kassim Manara na MAREHEMU Muhaji Mukhi,

Athumani Kilambo akiingia kwenye gari kurejea nyumbani mara baada ya kuruhusiwa kutoka kwenye Hospitali ya Ocean Road jijini Dar Es Salaam
Mwanachama wa Pan African Ndugu Yahya ambaye amekuwa naye bega kwa bega kuhakikisha anapona maradhi yanayomsumbua.
Hapa nipo na Mzee Kilambo nilipomtembelea Hospitalini kabla ya kuruhusiwa.

No comments:

Post a Comment